1 Kings 9:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na miji yake yote ya ghala, magari yake ya kukokotwa, na wapandafarasi wake; pia chochote alichotaka kujenga katika Yerusalemu, Lebanoni au kwingineko katika ufalme wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Vilevile, alijenga miji ya ghala na ya magari yake ya vita na kwa ajili ya farasi wake na wapanda farasi: alijenga kila alichotaka katika Yerusalemu, katika Lebanoni, na katika eneo lote alilotawala.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na miji yote ya hazina iliyokuwa yake Sulemani; na miji ya magari yake, na miji ya watu wake wapandao farasi, na kila alichopenda kujenga Sulemani huko Yerusalemu, na katika Lebanoni, na katika nchi yote ya mamlaka yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na miji yake yote ya ghala, magari yake ya kukokotwa, na wapandafarasi wake; pia chochote alichotaka kujenga katika Yerusalemu, Lebanoni au kwingineko katika ufalme wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
vile vile miji ya ghala na miji kwa ajili ya magari yake na farasi wake: cho chote alichotaka kujenga katika Yerusalemu, Lebanoni na katika nchi yote iliyokuwa chini ya mamlaka yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
vilevile miji ya ghala na miji kwa ajili ya magari yake na kwa ajili ya farasi wake: chochote alichotaka kujenga katika Yerusalemu, katika Lebanoni, na katika eneo yote aliyotawala.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na miji yote ya hazina iliyokuwa yake Sulemani; na miji ya magari yake, na miji ya watu wake wapandao farasi, na kila alichopenda kujenga Sulemani huko Yerusalemu, na katika Lebanoni, na katika nchi yote ya mamlaka yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
na miji yake yote ya ghala, magari yake ya kukokotwa, na wapandafarasi wake; pia chochote alichotaka kujenga katika Yerusalemu, Lebanoni au kwingineko katika ufalme wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
hata miji yote yenye vilimbiko, Salomo aliyokuwa nayo, nayo miji ya magari na miji ya farasi na majengo yote, Salomo aliyotaka kuyajenga kwa mapenzi yake mle Yerusalemu nake huko Libanoni na katika nchi yo yote ya ufalme wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na miji yote ya hazina iliyokuwa yake Sulemani; na miji ya magari yake, na miji ya watu wake wapandao farasi, na kila alichopenda kujenga Sulemani huko Yerusalemu, na katika Lebanoni, na katika nchi yote ya mamlaka yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
na miji yake yote ya kuwekea akiba, magari yake ya vita, na waaskari wapanda-farasi wake; vilevile na chochote alichotaka kujenga katika Yerusalema, Lebanoni au nafasi ingine katika ufalme wake.