1 Kings 9:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kati ya Waisraeli, Solomoni hakumfanya mtu yeyote kuwa mtumwa; wao ndio waliokuwa askari, watumishi wake, makamanda wake, maofisa wake, makamanda wa magari yake ya kukokotwa, na wapandafarasi wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Sulemani hakumfanya Mwisraeli yeyote kuwa mtumwa; hao ndio walikuwa wapiganaji wake, viongozi wa serikali yake, maafisa wake, wakuu wake wa jeshi, majemadari wa magari yake ya vita, na wapanda farasi wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini wa wana wa Israeli Sulemani hakumtumikisha mtu shokoa; ila ndio watu wa vita, na wangoje wake, na wakuu wake, na akida zake, na wakuu, wa magari yake, na wa wapanda farasi wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kati ya Waisraeli, Solomoni hakumfanya mtu yeyote kuwa mtumwa; wao ndio waliokuwa askari, watumishi wake, makamanda wake, maofisa wake, makamanda wa magari yake ya kukokotwa, na wapandafarasi wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Solomoni hakumfanya ye yote wa Waisraeli kuwa mtumwa; wao ndio waliokuwa wapiganaji wake, maafisa wake wa serikali, maafisa wake, wakuu wake, majemadari wa jeshi wa magari yake ya vita na wapanda farasi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Sulemani hakumfanya yeyote wa Waisraeli kuwa mtumwa; wao ndio waliokuwa wapiganaji wake, maafisa wake wa serikali, maafisa wake, wakuu wake, majemadari wa jeshi wa magari yake ya vita na wapanda farasi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini kwa wana wa Israeli Sulemani hakumtumikisha mtu yeyote shokoa; ila wao walikuwa askari, watumishi wake, makamanda wake, maafisa wake, makamanda wa magari yake na wapanda farasi wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kati ya Waisraeli, Solomoni hakumfanya mtu yeyote kuwa mtumwa; wao ndio waliokuwa askari, watumishi wake, makamanda wake, maofisa wake, makamanda wa magari yake ya kukokotwa, na wapandafarasi wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wana wa Isiraeli Salomo hakuwataka kuwa watumwa, kwani hawa walikuwa wapiga vita na watumishi wake na wakuu wake na wakuu wa thelathini na wakuu wa magari yake na wapanda farasi wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini wa wana wa Israeli Sulemani hakumtumikisha mtu shokoa; ila ndio watu wa vita, na wangoje wake, na wakuu wake, na akida zake, na wakuu, wa magari yake, na wa wapanda farasi wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kati ya Waisraeli, Solomono hakumufanya mutu hata mumoja kuwa mutumwa. Waisraeli walimutumikia kwa kuwa waaskari, waongozi, majemadari, wakubwa, wasimamizi wa magari yake ya vita, na waaskari wapanda-farasi.