1 Kings 9:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mara tatu kila mwaka, Solomoni alitoa tambiko za kuteketezwa na tambiko za amani juu ya madhabahu aliyokuwa amemjengea Mwenyezi-Mungu, akamfukizia Mwenyezi-Mungu ubani; pia alifanya marekebisho ya nyumba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sulemani akatoa dhabihu za kuteketezwa na sadaka za amani mara tatu kwa mwaka juu ya madhabahu aliyokuwa amemjengea Mwenyezi Mungu. Pamoja na hizo dhabihu, akafukiza uvumba mbele za Mwenyezi Mungu, hivyo kutimiza kanuni za Hekalu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mara tatu kila mwaka Sulemani alikuwa akitoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani juu ya madhabahu aliyomjengea Bwana akafukiza uvumba pamoja nazo juu ya madhabahu iliyokuwako mbele za Bwana. Hivyo akaimaliza nyumba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mara tatu kila mwaka, Solomoni alitoa tambiko za kuteketezwa na tambiko za amani juu ya madhabahu aliyokuwa amemjengea Mwenyezi-Mungu, akamfukizia Mwenyezi-Mungu ubani; pia alifanya marekebisho ya nyumba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Solomoni akatoa dhabihu za kuteketezwa na sadaka za amani mara tatu kwa mwaka, juu ya madhabahu aliyokuwa amejenga kwa ajili ya BWANA, akifukiza uvumba mbele za BWANA pamoja na dhabihu hizo, hivyo kutimiza kanuni za Hekalu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sulemani akatoa dhabihu za kuteketezwa na sadaka za amani mara tatu kwa mwaka, juu ya madhabahu aliyokuwa amejengea kwa ajili ya bwana, akifukiza uvumba mbele za bwana pamoja na dhabihu hizo, hivyo kutimiza kanuni za hekalu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mara tatu kila mwaka Sulemani alikuwa akitoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani juu ya madhabahu aliyomjengea BWANA akafukiza uvumba pamoja nazo juu ya madhabahu iliyokuwako mbele za BWANA. Hivyo akaimaliza nyumba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mara tatu kila mwaka, Solomoni alitoa tambiko za kuteketezwa na tambiko za amani juu ya madhabahu aliyokuwa amemjengea Mwenyezi-Mungu, akamfukizia Mwenyezi-Mungu ubani; pia alifanya marekebisho ya nyumba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Salomo akatoa kila mwaka mara tatu ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na za shukrani hapo pa kutambikia, alipomjengea Bwana; kila mara, alipozitoa, akavukiza penye meza iliyoko mbele ya Bwana. Alifanya hivyo alipokwisha kuimaliza hiyo Nyumba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mara tatu kila mwaka Sulemani alikuwa akitoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani juu ya madhabahu aliyomjengea BWANA akafukiza uvumba pamoja nazo juu ya madhabahu iliyokuwako mbele za BWANA. Hivyo akaimaliza nyumba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mara tatu kila mwaka, Solomono alitoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani juu ya mazabahu aliyokuwa amemujengea Yawe, akamufukizia Yawe ubani. Akafanya vile ilivyofaa kwa nyumba ya Yawe.