1 Kings 9:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
basi, nitawahamisha watu wangu, Israeli, kutoka nchi hii ambayo nimewapa; kadhalika na nyumba hii ambayo nimeiweka wakfu kwa ajili ya jina langu, nitaitupilia mbali nami, na kuifanya kitu cha kupuuzwa na kudharauliwa miongoni mwa mataifa yote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
basi nitakatilia mbali Israeli kutoka nchi niliyowapa, nami nitalikataa Hekalu hili nililolitakasa kwa ajili ya Jina langu. Ndipo Israeli itakuwa kitu cha kudharauliwa na watu na kuwa kitu cha kudhihakiwa miongoni mwa watu wote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
basi nitawakatilia Israeli mbali na nchi hii niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaitupilia mbali na macho yangu, na Israeli watakuwa mithali na neno la tusi katika mataifa yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
basi, nitawahamisha watu wangu, Israeli, kutoka nchi hii ambayo nimewapa; kadhalika na nyumba hii ambayo nimeiweka wakfu kwa ajili ya jina langu, nitaitupilia mbali nami, na kuifanya kitu cha kupuuzwa na kudharauliwa miongoni mwa mataifa yote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
basi nitakatilia mbali Israeli kutoka katika nchi niliyowapa na kulikataa Hekalu hili nililoliweka wakfu kwa Jina langu. Ndipo Israeli itakuwa kitu cha kudharauliwa na watu na kuwa kitu cha mzaha miongoni mwa watu wote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
basi nitakatilia mbali Israeli kutoka nchi niliyowapa, nami nitalikataa Hekalu hili nililolitakasa kwa ajili ya Jina langu. Ndipo Israeli itakuwa kitu cha kudharauliwa na watu na kuwa kitu cha kudhihakiwa miongoni mwa watu wote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
basi nitawakatilia Israeli mbali na nchi hii niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaitupilia mbali na macho yangu, na Israeli watakuwa mithali na neno la tusi katika mataifa yote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
basi, nitawahamisha watu wangu, Israeli, kutoka nchi hii ambayo nimewapa; kadhalika na nyumba hii ambayo nimeiweka wakfu kwa ajili ya jina langu, nitaitupilia mbali nami, na kuifanya kitu cha kupuuzwa na kudharauliwa miongoni mwa mataifa yote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ndipo, nitakapowang'oa Waisiraeli katika nchi hii, niliyowapa, nayo Nyumba hii, niliyoitakasa, iwe Kao la Jina langu, nitaiacha, macho yangu yasiione tena, nao Waisiraeli watakuwa fumbo na simango kwa makabila yote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
basi nitawakatilia Israeli mbali na nchi hii niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaitupilia mbali na macho yangu, na Israeli watakuwa mithali na neno la tusi katika mataifa yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
basi, nitawahamisha watu wangu, Waisraeli, kutoka inchi hii ambayo nimewapa; vilevile na nyumba hii ambayo niliyoitakasa kwa ajili ya jina langu, nitaitupilia mbali nami, na kuifanya kitu cha kuchekelewa na kuzarauliwa kati ya watu wa mataifa yote.