1 Kings 9:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na nyumba hii itabomoka na kuwa magofu; kila apitaye karibu atashtuka na kutikisa kichwa, na kuuliza, ‘Kwa nini Mwenyezi-Mungu amefanya hivyo kwa nchi hii na kwa nyumba hii?’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ingawa hekalu hili linavutia sasa, wote watakaolipita watashangaa na kudhihaki wakisema, ‘Kwa nini Mwenyezi Mungu amefanya kitu kama hiki katika nchi hii na kwa Hekalu hili?’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na ijapokuwa nyumba hii imetukuka namna hii, lakini kila apitaye atasituka na kuizomea; nao watasema, Kwa nini Bwana ameitenda nchi hii na nyumba hii mambo haya?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na nyumba hii itabomoka na kuwa magofu; kila apitaye karibu atashtuka na kutikisa kichwa, na kuuliza, ‘Kwa nini Mwenyezi-Mungu amefanya hivyo kwa nchi hii na kwa nyumba hii?’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ingawa Hekalu hili linavutia sasa, wote watakaopita karibu yake watashangaa na kudhihaki wakisema, ‘Kwa nini BWANA amefanya kitu cha namna hii katika nchi hii na kwenye Hekalu hili?’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ingawa hekalu hili linavutia sasa, wote watakaolipita watashangaa na kudhihaki wakisema, ‘Kwa nini bwana amefanya kitu kama hiki katika nchi hii na kwa Hekalu hili?’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na ijapokuwa nyumba hii imetukuka namna hii, lakini kila apitaye atashtuka na kuizomea; nao watasema, Kwa nini BWANA ameitenda nchi hii na nyumba hii mambo haya?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na nyumba hii itabomoka na kuwa magofu; kila apitaye karibu atashtuka na kutikisa kichwa, na kuuliza, ‘Kwa nini Mwenyezi-Mungu amefanya hivyo kwa nchi hii na kwa nyumba hii?’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nayo Nyumba hii iliyokuwa imetukuka kabisa, basi, kila atakayeipita ataistukia na kuizomea, waulize: Kwa sababu gani Bwana ameifanyizia hivi nchi hii na Nyumba hii?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na ijapokuwa nyumba hii imetukuka namna hii, lakini kila apitaye atasituka na kuizomea; nao watasema, Kwa nini BWANA ameitenda nchi hii na nyumba hii mambo haya?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na nyumba hii itaharibiwa na kuwa mabomoko. Kila mutu atakayepita karibu atashituka na kutikisa kichwa, na kuuliza: ‘Kwa nini Yawe amefanya hivyo kwa inchi hii na kwa nyumba hii?’