1 Peter 1:10 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Manabii walipeleleza na kufanya uchunguzi juu ya wokovu huo, wakabashiri juu ya neema hiyo ambayo nyinyi mngepewa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa habari ya wokovu huu, wale manabii waliosema kuhusu neema ambayo ingewafikia ninyi, walitafuta kwa bidii na kwa uangalifu mkubwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza, ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Manabii waliotabiri juu ya neema ambayo ingeoneshwa kwenu, walipeleleza kwa makini na kwa uangalifu wakaulizia habari za wokovu huu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Manabii walipeleleza kwa makini na kufanya uchunguzi juu ya wokovu huo, wakabashiri juu ya neema hiyo ambayo ninyi mngepewa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Manabii walipeleleza na kufanya uchunguzi juu ya wokovu huo, wakabashiri juu ya neema hiyo ambayo nyinyi mngepewa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa habari ya wokovu huu, wale manabii waliosema kuhusu neema ambayo ingewajia ninyi, walitafuta kwa bidii na kwa uangalifu mkubwa,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa habari ya wokovu huu, wale manabii waliosema kuhusu neema ambayo ingewajia ninyi, walitafuta kwa bidii na kwa uangalifu mkubwa,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kuhusu wokovu huo, manabii ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi, walichunguza sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Manabii walipeleleza na kufanya uchunguzi juu ya wokovu huo, wakabashiri juu ya neema hiyo ambayo nyinyi mngepewa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wafumbuaji walioyafumbua hayo mema, mliyogawiwa, waliutafuta sana wokovu huo na kuuchunguza; wakayafuatafuata, wapate kujua,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika habari ya wokovu huo manabii walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza, ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Manabii walifanya uchunguzi na upelelezi juu ya wokovu ule, nao walitabiri juu ya zawadi ambayo ninyi mungepewa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Katika khabari ya wokofu huo walitafutatafuta na kuchunguzachunguza manabii waliotabiri khabari va neema itakayowafikia,