1 Peter 1:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walijaribu kujua nyakati na mazingira ya tukio hilo, yaani wakati alioudokezea Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, akibashiri juu ya mateso yatakayompata Kristo na utukufu utakaofuata.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walijaribu kujua ni wakati upi na ni mazingira yapi ambayo Roho wa Al-Masihi, aliyekuwa ndani yao, alionesha alipotabiri mateso ya Al-Masihi na utukufu ambao ungefuata.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Roho wa Kristo alikuwa ndani yao, naye aliwapa ushuhuda mapema kuhusu Kristo kwamba itamlazimu kuteswa na baada ya hapo atapokea utukufu. Manabii waliuliza kutaka kujua wakati gani na katika mazingira gani mambo haya yangetokea.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Walijaribu kujua nyakati na mazingira ya tukio hilo, yaani wakati alioudokezea Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, akibashiri juu ya mateso yatakayompata Kristo na utukufu utakaofuata.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walijaribu kujua nyakati na mazingira ya tukio hilo, yaani wakati alioudokezea Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, akibashiri juu ya mateso yatakayompata Kristo na utukufu utakaofuata.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
wakijaribu kujua ni wakati upi na katika mazingira gani ambayo Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao alionyesha alipotabiri kuhusu mateso ya Kristo na utukufu ule ambao ungefuata.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
wakijaribu kujua ni wakati upi na katika mazingira gani ambayo Roho wa Al-Masihi aliyekuwa ndani yao alionyesha, alipotabiri kuhusu mateso ya Al-Masihi na utukufu ule ambao ungefuata.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walijaribu kujua nyakati na mazingira ya tukio hilo, yaani wakati alioudokezea Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, akibashiri juu ya mateso yatakayompata Kristo na utukufu utakaofuata.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kama ni siku za wakati gani zile, ambazo Roho ya Kristo, waliyokuwa nayo, inazivumbua na kuyashuhudia hapo kale mateso yatakayompata Kristo nao utukufu utakaokuwa mwishoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao alitangulia kushuhudia mateso yatakayomupata Kristo na utukufu utakaokuwa nyuma. Nao walijitolea kusudi wapate kuvumbua wakati gani na kwa njia gani mambo haya yatafanyika.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
wakitafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho ya Kristo iliyokuwa ndaui yao, aliyetangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwa baada ya hayo.