1 Peter 1:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnapomtaja Mungu, nyinyi humwita Baba. Basi, jueni kwamba yeye humhukumu kila mmoja kadiri ya matendo yake, bila ubaguzi. Hivyo tumieni wakati wenu uliowabakia hapa ugenini katika kumcha Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa mnamlilia Baba anayehukumu kila mtu kulingana na matendo yake pasipo upendeleo, kaeni kama wageni wakati wenu duniani, mkiogopa na kumcha Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na kama Baba mnayemwita Mungu anayewahukumu watu bila upendeleo kwa kadri ya matendo ya kila mtu, muishi maisha ya utauwa na hofu kwa Mungu katika miaka yenu ya kukaa humu duniani kama wageni.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mnapomtaja Mungu ninyi humwita Baba. Basi, jueni kwamba yeye humhukumu kila mmoja kadiri ya matendo yake, bila ubaguzi. Hivyo tumieni wakati wenu uliowabakia hapa ugenini katika kumcha Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnapomtaja Mungu, nyinyi humwita Baba. Basi, jueni kwamba yeye humhukumu kila mmoja kadiri ya matendo yake, bila ubaguzi. Hivyo tumieni wakati wenu uliowabakia hapa ugenini katika kumcha Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nanyi kama mnamwita Baba yeye ahukumuye kila mtu kulingana na matendo yake pasipo upendeleo, enendeni kwa hofu ya kumcha Mungu wakati wenu wa kukaa hapa duniani kama wageni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa sababu mnamwita Baba ahukumuye kila mtu kulingana na matendo yake pasipo upendeleo, enendeni kwa hofu ya kumcha Mungu wakati wenu wa kukaa hapa duniani kama wageni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, nendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mnapomtaja Mungu, nyinyi humwita Baba. Basi, jueni kwamba yeye humhukumu kila mmoja kadiri ya matendo yake, bila ubaguzi. Hivyo tumieni wakati wenu uliowabakia hapa ugenini katika kumcha Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Tena ninyi humwita Baba yeye anayemhukumu kila mtu kwa kazi yake pasipo kupendelea; kwa hiyo mwendelee miaka yenu ya kukaa ugenini na kuogopa!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na ikiwa katika maombi yenu munamwita “Baba” yule anayehukumu kila mutu pasipo upendeleo kufuatana na matendo yake, basi muishi katika heshima mbele yake kwa muda unaowabakilia kwa kuishi hapa katika dunia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na ikiwa mnamwita Baba yeye ahukumuye killa mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa khofu kafika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni;