1 Peter 1:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana mnajua kwamba nyinyi mlikombolewa katika mwenendo wenu usiofaa ambao mliupokea kutoka kwa wazee wenu. Lakini hamkukombolewa kwa vitu vyenye kuharibika: Kwa fedha na dhahabu;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana mnafahamu kwamba mlikombolewa kutoka mwenendo wenu usiofaa, ambao mliurithi kutoka kwa baba zenu. Hamkukombolewa kwa vitu viharibikavyo kama fedha na dhahabu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mnajua kwamba siyo kwa mambo yaharibikayo kama fedha au dhahabu, kwamba mliokolewa kutoka katika maisha yasiyofaa mliyoyapokea kutoka kwa babu zenu,
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana mnajua kwamba ninyi mlikombolewa katika mwenendo wenu usiofaa ambao mliupokea kutoka kwa wazee wenu, si kwa vitu vyenye kuharibika: kwa fedha na dhahabu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana mnajua kwamba nyinyi mlikombolewa katika mwenendo wenu usiofaa ambao mliupokea kutoka kwa wazee wenu. Lakini hamkukombolewa kwa vitu vyenye kuharibika: kwa fedha na dhahabu;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana mnafahamu kwamba mlikombolewa kutoka katika mwenendo wenu usiofaa ambao mliurithi kutoka kwa baba zenu, si kwa vitu viharibikavyo, yaani, kwa fedha na dhahabu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana mnafahamu kwamba mlikombolewa kutoka mwenendo wenu usiofaa ambao mliurithi kutoka kwa baba zenu, si kwa vitu viharibikavyo kama fedha na dhahabu,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana mnajua kwamba nyinyi mlikombolewa katika mwenendo wenu usiofaa ambao mliupokea kutoka kwa wazee wenu. Lakini hamkukombolewa kwa vitu vyenye kuharibika: Kwa fedha na dhahabu;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jueni: vyenye kuoza, vingawa fedha au dhahabu, sivyo, ambavyo mlikombolewa navyo katika mwenendo wenu wa kikale uliokuwa hauna maana;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana munajua namna gani mulivyokombolewa toka katika tabia za ovyo ovyo mulizoambukizwa na babu zenu. Hamukukombolewa kwa njia ya vitu vinavyoharibika kama vile feza au zahabu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
mkijua kwamba hamkukombolewa kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu, mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlionpokea kwa baba zenu;