1 Peter 1:19 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
bali kwa damu ya thamani ya Kristo, ambaye alikuwa kama mwanakondoo asiye na dosari wala doa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
bali mlikombolewa kwa damu ya thamani ya Al-Masihi, yule Mwana-Kondoo asiye na dosari wala doa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
bali kwa damu ya thamani ya Kristo, kama ile ya mwanakondoo asiye na dosari wala ila.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
bali mlikombolewa kwa damu tukufu ya Kristo, ambaye alikuwa kama mwana kondoo asiye na dosari wala doa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
bali kwa damu ya thamani ya Kristo, ambaye alikuwa kama mwanakondoo asiye na dosari wala doa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
bali kwa damu ya thamani ya Kristo, kama ile ya Mwana-Kondoo asiye na dosari wala doa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bali kwa damu ya thamani ya Al-Masihi, yule Mwana-Kondoo asiye na dosari wala doa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na dosari wala waa, yaani, ya Kristo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
bali kwa damu ya thamani ya Kristo, ambaye alikuwa kama mwanakondoo asiye na dosari wala doa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ila mmekombolewa kwa damu ya Kristo iliyo yenye kima kikuu, maana alikuwa mwana kondoo asiye na kilema wala doadoa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini mulikombolewa kwa njia ya damu yenye bei kali ya Kristo, aliyekuwa kama kondoo asiyekuwa na kilema wala uchafu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana kondoo asio na ila, na asio na waa, ya Kristo,