1 Peter 1:2 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu Baba aliwateua nyinyi kufuatana na kusudi lake, na mmefanywa watakatifu na Roho, mpate kumtii Yesu Kristo na kusafishwa kwa damu yake. Nawatakieni neema na amani tele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni ninyi ambao mlichaguliwa tangu mwanzo na Mungu Baba Mwenyezi kulingana na alivyotangulia kuwajua, kupitia kwa kazi ya utakaso wa Roho wa Mungu, katika utiifu kwa Isa Al-Masihi na kunyunyiziwa damu yake. Neema na amani ziwe kwenu kwa wingi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kununyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa kadri ya mpango wa Mungu Baba alioufanya muda mrefu uliopita, mliteuliwa muwe wake kwa kufanywa watakatifu na Roho Mtakatifu. Mliteuliwa kuwa waatiifu kwa Mungu na kutakaswa na kujumuishwa miongoni mwa watu wa Agano Jipya kwa kunyunyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani ya Mungu viwe pamoja nanyi kwa wingi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mungu Baba aliwateua ninyi kufuatana na kusudi lake, na mmefanywa watakatifu na Roho, mpate kumtii Yesu Kristo na kusafishwa kwa damu yake. Nawatakieni neema na amani tele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu Baba aliwateua nyinyi kufuatana na kusudi lake, na mmefanywa watakatifu na Roho, mpate kumtii Yesu Kristo na kusafishwa kwa damu yake. Nawatakieni neema na amani tele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ninawaandikia ninyi ambao mlichaguliwa tangu mwanzo na Mungu Baba kulingana na alivyotangulia kuwajua, kwa kazi ya utakaso wa Roho, katika utii na kunyunyizwa damu ya Yesu Kristo: Neema iwe nanyi na amani iongezwe kwenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni ninyi ambao mlichaguliwa tangu mwanzo na Mungu Baba kulingana na alivyotangulia kuwajua, kupitia kwa kazi ya utakaso wa Roho wa Mwenyezi Mungu, katika utiifu kwa Isa Al-Masihi na kunyunyiziwa damu yake: Neema na amani ziwe kwenu kwa wingi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kunyunyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu Baba aliwateua nyinyi kufuatana na kusudi lake, na mmefanywa watakatifu na Roho, mpate kumtii Yesu Kristo na kusafishwa kwa damu yake. Nawatakieni neema na amani tele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hivyo, Mungu Baba alivyowatambua kale, aliwatakasa kwa Roho yake, mpate kutii kwa kunyunyizwa damu yake Yesu Kristo. Upole uwafurikie na utengemano!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kununyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu Baba aliwachagua ninyi tangu mbele kufuatana na mupango wake na kufanywa watakatifu na Roho, mupate kumutii Yesu Kristo na kusafishwa kwa damu yake. Ninawatakia neema na amani kwa uwingi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kama vile Mungu alivyotangulia kuwajua tangu milele katika utakaso wa Roho, hatta wakapata kutii na kunyunyizwa damu ya Yesu Kristo; Neema na amani ziongezwe kwenu.