1 Peter 1:22 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maadamu sasa, kwa kuutii ukweli, nyinyi mmezitakasa roho zenu na kuwapenda wenzenu bila unafiki, basi, pendaneni kwa moyo wote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi kwa kuwa mmejitakasa nafsi zenu kwa kuitii ile kweli hata mkawa na upendo wa ndugu usio na unafiki, basi pendaneni kwa dhati kutoka moyoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sasa kwa vile mmejitakasa wenyewe kwa kuitii kweli hadi mwisho kwamba mtaonesha upendo wa kweli wa kindugu, jitahidini kupendana ninyi kwa ninyi kwa mioyo iliyo safi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maadamu sasa, kwa kuutii ukweli, ninyi mmezitakasa roho zenu na kuwapenda wenzenu bila unafiki, basi, pendaneni kwa moyo wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maadamu sasa, kwa kuutii ukweli, nyinyi mmezitakasa roho zenu na kuwapenda wenzenu bila unafiki, basi, pendaneni kwa moyo wote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi kwa kuwa mmejitakasa nafsi zenu kwa kuitii ile kweli kwa njia ya Roho kwa kuwapenda ndugu zenu kwa upendo wa kweli, pendaneni kwa dhati kutoka moyoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi kwa kuwa mmejitakasa nafsi zenu kwa kuitii ile kweli hata mkawa na upendo wa ndugu usio na unafiki, basi pendaneni kwa dhati kutoka moyoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo safi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maadamu sasa, kwa kuutii ukweli, nyinyi mmezitakasa roho zenu na kuwapenda wenzenu bila unafiki, basi, pendaneni kwa moyo wote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa kuwa mmezitakasa roho zenu na kuyatii yaliyo ya kweli, pendaneni kindugu pasipo ujanja mkijikaza kupendana kila mtu na mwenziwe kwa moyo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninyi mumekwisha kutakaswa kwa njia ya kutii neno la kweli kwa kuwapenda wandugu zenu pasipo unafiki. Basi mupendane kabisa, kwa moyo wenu wote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mkiisha kujisafisha roho zenu kwa kuitii kweli, kwa Roho, kiasi cha kuufikilia upendano usio na unafiki, bassi jitahidini kupendana kwa moyo;