1 Peter 1:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana kwa njia ya neno hai la Mungu, nyinyi mmezaliwa upya, si kama watoto wa baba awezaye kufa, bali baba asiyekufa milele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana mmezaliwa upya, si kwa mbegu inayoharibika, bali kwa mbegu isiyoharibika, kupitia kwa neno la Mungu lililo hai na linalodumu milele.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mmezaliwa upya sio kama matokeo ya mbegu inayoharibika, lakini kama matokeo ya mbegu isiyoharibika. Mmezaliwa upya kwa njia ya ujumbe wa Mungu, ambao unaleta uzima ndani yenu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana kwa njia ya neno hai la Mungu, ninyi mmezaliwa upya, si kama watoto wa baba awezaye kufa, bali baba asiyekufa milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana kwa njia ya neno hai la Mungu, nyinyi mmezaliwa upya, si kama watoto wa baba awezaye kufa, bali baba asiyekufa milele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana mmezaliwa upya, si kwa mbegu ile iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika, kwa neno la Mungu lililo hai na linalodumu hata milele.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana mmezaliwa upya, si kwa mbegu ile iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika, kupitia kwa neno la Mwenyezi Mungu lililo hai na linalodumu milele.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, linalodumu hata milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana kwa njia ya neno hai la Mungu, nyinyi mmezaliwa upya, si kama watoto wa baba awezaye kufa, bali baba asiyekufa milele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mkiwa mmezaliwa mara ya pili, siyo nguvu ya mbegu iozayo, ila ni nguvu ya mbegu isiyoozeka, ndiyo Neno la Mungu lililo lenye uzima, nalo ndilo likaalo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana mumezaliwa upya, kwa nguvu za neno la Mungu lenye uzima na linalodumu hata milele. Nanyi si kama watoto waliozaliwa na wazazi wenye mwili huu unaokuwa wa kufa, lakini watoto waliozaliwa kwa nguvu ya uzazi usioweza kufa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kwa kuwa mmezaliwa marra ya pili, si kwa mbegu iharibikayo, bali isiyoharibika, kwa neno la Mungu lenye uzima, na lidumulo hatta milele.