1 Peter 1:24 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama Maandiko yasemavyo: “Kila binadamu ni kama majani, na utukufu wake wote ni kama ua la majani. Majani hunyauka na maua huanguka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Maana, “Wanadamu wote ni kama majani, nao utukufu wao wote ni kama maua ya kondeni; majani hunyauka na maua huanguka,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana, Mwili wote ni kama majani, Na fahari yake yote ni kama ua la majani. Majani hukauka na ua lake huanguka;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo, kama Maandiko yanavyosema: “Watu wote ni kama manyasi, na utukufu wao wote ni kama maua pori katika manyasi. Manyasi yananyauka na kukauka, na maua yanapukutika,
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kama Maandiko yasemavyo: “Kila binadamu ni kama nyasi, na utukufu wake wote ni kama maua ya porini. Nyasi hunyauka na maua huanguka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama Maandiko yasemavyo: “Kila binadamu ni kama majani, na utukufu wake wote ni kama ua la majani. Majani hunyauka na maua huanguka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Maana, “Watu wote ni kama majani, na utukufu wao ni kama ua la shambani; majani hunyauka na ua lake hupukutika,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Maana, “Wanadamu wote ni kama majani, nao utukufu wao ni kama maua ya kondeni; majani hunyauka na maua huanguka,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana, Mwili wote ni kama majani, Na fahari yake yote ni kama ua la majani. Majani hukauka na ua lake huanguka;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama Maandiko yasemavyo: “Kila binadamu ni kama majani, na utukufu wake wote ni kama ua la majani. Majani hunyauka na maua huanguka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani kila mwenye mwili ni kama majani, nao uzuri wake wote ni kama ua la majani. Majani hunyauka, nayo maua yake hupukutika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana, Mwili wote ni kama majani, Na fahari yake yote ni kama ua la majani. Majani hukauka na ua lake huanguka;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana Maandiko Matakatifu yanasema: “Wanadamu wote ni kama majani. Na utukufu wao wote unatoweka kama maua. Majani yanakauka na maua yanaanguka.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana, Mwili wote kama majani, Na utukufu wake wote kama ua la majaui. Majani hukauka na ua lake huanguka;