1 Peter 1:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Furahini kuhusu jambo hilo, ijapokuwa sasa, kwa kitambo kidogo, itawabidi kuhuzunika kwa sababu ya majaribio mbalimbali mnayoteseka,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika haya yote mnafurahi sana, ijapokuwa kwa muda mfupi sasa mmehuzunishwa kwa majaribu ya aina nyingi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hili linawafanya mfurahi sana, hata kama kwa sasa imewalazimu mhuzunishwe kwa kipindi kifupi kwa masumbufu na mateso ya aina mbali mbali.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Furahini kuhusu jambo hilo, ijapokuwa sasa, kwa kitambo kidogo, itawabidi kuhuzunika kwa sababu ya majaribio mbalimbali mnayoteseka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Furahini kuhusu jambo hilo, ijapokuwa sasa, kwa kitambo kidogo, itawabidi kuhuzunika kwa sababu ya majaribio mbalimbali mnayoteseka,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika hili mnafurahi sana, ingawa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna nyingi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika hili mnafurahi sana, ingawa sasa kwa kitambo kidogo mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna nyingi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa muda mfupi, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Furahini kuhusu jambo hilo, ijapokuwa sasa, kwa kitambo kidogo, itawabidi kuhuzunika kwa sababu ya majaribio mbalimbali mnayoteseka,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo mtashangilia, hata ikiwapasa sasa kusikitika siku kidogo, mkijaribiwa na mambo menginemengine,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika mambo hayo yote mushangilie kwa furaha ijapokuwa inawapasa sasa kuhuzunika kwa wakati kidogo kwa ajili ya majaribu ya namna mbalimbali.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mnafurahi sana kwa ajili yake, ijapokuwa sasa kwa kitambo, ikiwa ni lazima, mmchuzunishwa kwa majaribu ya namna mbali mbali,