1 Peter 1:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
majaribio ambayo shabaha yake ni kuthibitisha imani yenu. Hata dhahabu yenyewe, ambayo huharibika, hujaribiwa kwa moto; hali kadhalika na imani yenu, ambayo ni ya thamani kuliko dhahabu, ni lazima ijaribiwe ipate kuwa thabiti. Hapo mtapokea sifa na utukufu na heshima siku ile Yesu Kristo atakapofunuliwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Haya yamewajia ili imani yenu, iliyo ya thamani kuliko dhahabu ipoteayo ingawa inasafishwa kwa moto, ionekane kuwa halisi, na imalizie kwa sifa, utukufu na heshima Isa Al-Masihi atakapodhihirishwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa masumbufu haya imani yenu inajaribiwa na kuithibitishwa kuwa ni ya kweli. Hii inafananishwa na dhahabu pale inapopitishwa kwenye moto kuthibitisha uhalisi wake. Lakini hata dhahabu ya kweli inaweza kuharibiwa. Hivyo imani ina thamani zaidi kuliko dhahabu. Pale imani yenu inapothibitika kuwa ni ya kweli, matokeo yake ni sifa, utukufu na heshima kwa Mungu wakati wa kurudi kwake Yesu Kristo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Shabaha yake ni kuthibitisha imani yenu. Hata dhahabu yenyewe ambayo huharibika, hujaribiwa kwa moto; hali kadhalika na imani yenu ambayo ni ya thamani zaidi kuliko dhahabu, ni lazima ijaribiwe ipate kuwa thabiti. Hapo mtapokea sifa na utukufu na heshima Siku ile Yesu Kristo atakapofunuliwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
majaribio ambayo shabaha yake ni kuthibitisha imani yenu. Hata dhahabu yenyewe, ambayo huharibika, hujaribiwa kwa moto; hali kadhalika na imani yenu, ambayo ni ya thamani kuliko dhahabu, ni lazima ijaribiwe ipate kuwa thabiti. Hapo mtapokea sifa na utukufu na heshima siku ile Yesu Kristo atakapofunuliwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Haya yamewajia ili kwamba uhalisi wa imani yenu (yenye thamani kuliko dhahabu ipoteayo, ingawa hujaribiwa kwa moto) ionekane kuwa katika sifa, utukufu na heshima wakati Yesu Kristo atakapodhihirishwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Haya yamewajia ili kwamba imani yenu, iliyo ya thamani kuliko dhahabu ipoteayo, ingawa hujaribiwa kwa moto, ionekane kuwa halisi na imalizie katika sifa, utukufu na heshima wakati Isa Al-Masihi atadhihirishwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
majaribio ambayo shabaha yake ni kuthibitisha imani yenu. Hata dhahabu yenyewe, ambayo huharibika, hujaribiwa kwa moto; hali kadhalika na imani yenu, ambayo ni ya thamani kuliko dhahabu, ni lazima ijaribiwe ipate kuwa thabiti. Hapo mtapokea sifa na utukufu na heshima siku ile Yesu Kristo atakapofunuliwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kwamba: Kumtegemea Mungu kujulike kwenu kuwa kwa kweli, kisha kuonekane kuwa kwenye kima sana kuliko dhahabu iangamikayo, nayo uzuri wake hujulikana motoni. Mkiwa hivyo mtapata sifa na utukufu na macheo hapo, Yesu Kristo atakapotokea waziwazi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Majaribu hayo ni kwa ajili ya kupima imani yenu. Zahabu ni kitu kinachoharibika, lakini ingawa vile inapimwa kwa njia ya kuchomwa ndani ya moto. Hivi vilevile imani yenu inayokuwa ya bei kali kuliko zahabu, inapaswa kupimwa kusudi ijulikane kuwa ya kweli. Na kwa sababu hii mutapata sifa, utukufu na heshima wakati Yesu Kristo atakapotokea.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
illi kujaribiwa kwake imani yenu, ambako kuna thamani kuu kuliko dbahabu ipoteayo, ijapokuwa imejaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo: