1 Peter 2:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenendo wenu kati ya watu wasiomjua Mungu unapaswa kuwa mwema kabisa, ili hata watakapowasingizieni kwamba mnatenda mabaya, waweze kutambua matendo yenu mema na hivyo wamtukuze Mungu siku ya kuja kwake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuweni na mwenendo mzuri mbele ya watu wasiomjua Mungu, ili kama wanawasingizia kuwa watenda mabaya, wayaone matendo yenu mema nao wamtukuze Mungu siku atakapokuja kwetu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Muwe na uhakika wa kuwa na mwenendo mzuri mbele ya wapagani, ili hata kama wakiwalaumu kama wakosaji, watayaona matendo yenu mazuri nao wanaweza kumpa Mungu utukufu katika Siku ya kuja kwake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mwenendo wenu kati ya watu wasiomjua Mungu unapaswa kuwa mwema kabisa, ili hata watakapowasingizieni kwamba mnatenda mabaya, waweze kutambua matendo yenu mema na hivyo wamtukuze Mungu Siku ya kuja kwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenendo wenu kati ya watu wasiomjua Mungu unapaswa kuwa mwema kabisa, ili hata watakapowasingizieni kwamba mnatenda mabaya, waweze kutambua matendo yenu mema na hivyo wamtukuze Mungu siku ya kuja kwake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwe na mwenendo mzuri mbele ya watu wasiomjua Mungu, ili kama wanawasema kuwa ninyi ni watenda mabaya, wayaone matendo yenu mema wamtukuze Mungu siku atakapokuja kuhukumu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuweni na mwenendo mzuri mbele ya watu wasiomjua Mungu, ili kama wanawasingizia kuwa watenda mabaya, wayaone matendo yenu mema nao wamtukuze Mwenyezi Mungu siku atakapokuja kwetu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Muwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenendo wenu kati ya watu wasiomjua Mungu unapaswa kuwa mwema kabisa, ili hata watakapowasingizieni kwamba mnatenda mabaya, waweze kutambua matendo yenu mema na hivyo wamtukuze Mungu siku ya kuja kwake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Fanyeni mwenendo ulio mzuri kwa wamizimu! Hivyo wale wanaowasingizia ninyi kuwa watenda maovu, wanapoziona kazi zenu nzuri, watamtukuza Mungu siku ile, atakapowatokea kuwakagua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mukuwe na mwenendo muzuri kati ya wapagani, kusudi wakiwasingizia kwamba mumefanya mabaya, wapate kuona matendo yenu mema na wamutukuze Mungu siku ile ya kuja kwake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
mwe na maongezi mazuri kati ya Mataifa, illi, iwapo huwasingizia kuwa mnatenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa nae.