1 Peter 2:20 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana, mtapata tuzo gani mkivumilia mapigo mnayostahili kwa sababu ya makosa yenu? Lakini kama mnavumilia mateso hata ingawa mmetenda mema, Mungu atawapeni baraka kwa ajili hiyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwani ni faida gani kwa mtu kustahimili anapopigwa kwa sababu ya makosa yake? Lakini mkiteswa kwa sababu ya kutenda mema, nanyi mkastahimili, hili ni jambo la kusifiwa mbele za Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana ni sifa gani kustahimili, mtendapo dhambi na kupigwa makofi? Lakini kustahimili, mtendapo mema na kupata mateso, huu ndio wema hasa mbele za Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwani kuna sifa gani iliyopo kwako kama utapigwa kwa kutenda mabaya na kuvumilia? Lakini kama utateseka kwa kutenda mema na kustahimili, hili lampendeza Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana, mtapata tuzo gani mkivumilia mapigo mnayostahili kwa sababu ya makosa yenu? Lakini kama mnavumilia mateso hata ingawa mmetenda mema, Mungu atawapeni baraka kwa ajili hiyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana, mtapata tuzo gani mkivumilia mapigo mnayostahili kwa sababu ya makosa yenu? Lakini kama mnavumilia mateso hata ingawa mmetenda mema, Mungu atawapeni baraka kwa ajili hiyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwani ni faida gani kwa mtu kustahimili anapopigwa kwa sababu ya makosa yake? Lakini kama mkiteswa kwa sababu ya kutenda mema, nanyi mkastahimili, hili ni jambo la sifa mbele za Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwani ni faida gani kwa mtu kustahimili anapopigwa kwa sababu ya makosa yake? Lakini kama mkiteswa kwa sababu ya kutenda mema, nanyi mkastahimili, hili ni jambo la kusifiwa mbele za Mwenyezi Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana ni sifa gani kustahimili, mtendapo dhambi na kupigwa makofi? Lakini kustahimili, mtendapo mema na kupata mateso, huu ndio wema hasa mbele za Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana, mtapata tuzo gani mkivumilia mapigo mnayostahili kwa sababu ya makosa yenu? Lakini kama mnavumilia mateso hata ingawa mmetenda mema, Mungu atawapeni baraka kwa ajili hiyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani ni chema gani cha kukivumisha, mkiyavumilia mapigo, myapatayo kwa sababu ya kukosa? Lakini mkiyavumilia mateso yawapatayo kwa sababu ya kutenda mema, hiki ndicho chema, Mungu alichowagawia.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana ni sifa gani kustahimili, mtendapo dhambi na kupigwa makofi? Lakini kustahimili, mtendapo mema na kupata mateso, huu ndio wema hasa mbele za Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuna sifa gani kama mukivumilia mapigo kwa sababu mulitenda mabaya? Lakini mukivumilia mateso kwa sababu mulitenda mema, jambo hilo linamupendeza Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana ni sifa gani kuvumilia, mtendapo dhambi na kupigwa makofi? Lakini kuvumilia, mtendapo mema na kupata mateso, huu ndio wema khassa mbele za Mungu.