1 Peter 2:4 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, mwendeeni Bwana! Yeye ndiye jiwe hai lililokataliwa na watu; lakini mbele ya Mungu ni jiwe teule na la thamani kubwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mnapokuja kwake, yeye aliye Jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu bali kwa Mungu ni teule na la thamani kwake,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mkaribieni Bwana Yesu, aliye Jiwe lililo Hai, lililokataliwa na watu, bali kwa Mungu ni jiwe lililoteuliwa na kuheshimika.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, mwendeeni Bwana! Yeye ndiye jiwe hai lililokataliwa na watu; lakini mbele ya Mungu ni jiwe teule, na la thamani kubwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, mwendeeni Bwana! Yeye ndiye jiwe hai lililokataliwa na watu; lakini mbele ya Mungu ni jiwe teule na la thamani kubwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwendeeni yeye aliye Jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu bali kwa Mungu ni teule na la thamani kwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mnapokuja kwake, yeye aliye Jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu bali kwa Mwenyezi Mungu ni teule na la thamani kwake,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, mwendeeni Bwana! Yeye ndiye jiwe hai lililokataliwa na watu; lakini mbele ya Mungu ni jiwe teule na la thamani kubwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huyu mjieni! Maana ni jiwe lenye uzima. Kweli watu walilikataa, lakini Mungu amelichagua kuwa lenye heshima.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mumwendee Bwana. Yeye ni jiwe lenye uzima. Jiwe lile lilitupiliwa na watu lakini lilichaguliwa na Mungu, nalo linahesabiwa kuwa la bei kali mbele yake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mkimwendea yeye, jiwe lililo hayi, lililokataliwa na wana Adamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye thamani,