1 Peter 2:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana Maandiko Matakatifu yasema: “Tazama! Naweka jiwe huko Siyoni, jiwe la msingi, teule na la thamani. Mtu atakayemwamini huyo hataaibishwa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana imeandikwa katika Maandiko: “Tazama, naweka katika Sayuni, jiwe la pembeni teule lenye thamani, na yeyote atakayemwamini hataaibishwa kamwe.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo, Maandiko yanasema, “Tazameni, naweka katika Sayuni Jiwe la msingi katika jengo, lililoteuliwa na kuheshimika, na yeyote anayeamini hataaibishwa.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana Maandiko Matakatifu yasema: “Tazama! Naweka huko sioni jiwe kuu la msingi, jiwe la thamani kubwa nililoliteua. Mtu atakayemwamini yeye aliye hilo jiwe, hataaibishwa.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana Maandiko Matakatifu yasema: “Tazama! Naweka jiwe huko Siyoni, jiwe la msingi, teule na la thamani. Mtu atakayemwamini huyo hataaibishwa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana Andiko lasema: “Tazama, naweka katika Sayuni, Jiwe Kuu la pembeni, teule lenye thamani, na kila amwaminiye hataaibika.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana imeandikwa katika Maandiko: “Tazama, naweka katika Sayuni, jiwe la pembeni teule lenye thamani, na yeyote atakayemwamini hataaibika kamwe.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa imeandikwa katika Maandiko: Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana Maandiko Matakatifu yasema: “Tazama! Naweka jiwe huko Siyoni, jiwe la msingi, teule na la thamani. Mtu atakayemwamini huyo hataaibishwa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo imeandikwa katika Maandiko kwamba: Tazameni, naweka humu Sioni jiwe la pembeni lililochaguliwa kuwa lenye heshima, naye alitegemeaye hatatwezeka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa kuwa imeandikwa hivi katika Maandiko Matakatifu: “Nimesimika jiwe kubwa la pembe katika Sayuni, jiwe lile ni la bei kali. Ni mimi niliyelichagua. Yule anayelitumainia hatapata haya.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa kuwa ndiyo yaliyomo katika maandiko, Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye thamani, Na killa amwaminiye hatatabayarika.