1 Peter 2:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwenu nyinyi mnaoamini, jiwe hilo ni la thamani kubwa; lakini kwa wale wasioamini, “Jiwe walilolikataa waashi, sasa limekuwa jiwe kuu la msingi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwenu ninyi mnaoamini, jiwe hili ni la thamani. Lakini kwao wasioamini, “Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni,”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Inamaanisha heshima kwenu mnaoamini, bali kwa wasioamini, “jiwe walilolikataa wajenzi limekuwa jiwe la muhimu kuliko yote.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwenu ninyi mnaoamini, jiwe hilo ni la thamani kubwa; lakini kwa wale wasioamini, “Jiwe walilokataa waashi, sasa limekuwa jiwe kuu la msingi.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwenu nyinyi mnaoamini, jiwe hilo ni la thamani kubwa; lakini kwa wale wasioamini, “Jiwe walilolikataa waashi, sasa limekuwa jiwe kuu la msingi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwenu ninyi mnaoamini, yeye ni wa thamani. Lakini kwao wasioamini, “Jiwe lile walilolikataa waashi limekuwa Jiwe Kuu la pembeni,”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwenu ninyi mnaoamini, jiwe hili ni la thamani. Lakini kwao wasioamini, “Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni,”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini, Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwenu nyinyi mnaoamini, jiwe hilo ni la thamani kubwa; lakini kwa wale wasioamini, “Jiwe walilolikataa waashi, sasa limekuwa jiwe kuu la msingi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo ninyi mlitegemealo hupata heshima, lakini wasiolitegemea jiwe hili, waashi walilolikataa, hilihili huwa kwao jiwe la pembeni kwamba:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini, Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi jiwe lile linahesabiwa kuwa la bei kali kwa wale wanaoamini. Lakini kwa wale wasioamini ni: “Jiwe lililotupiliwa na wajengaji, lakini sasa linakuwa jiwe kubwa la pembe.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi, thamani hii ni kwenu ninyi mnaoamini, bali kwao wasioamini, Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni;