1 Peter 3:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nanyi wake, jiwekeni chini ya mamlaka ya waume zenu, ili kama wako waume wowote wasioamini neno la Mungu, wapate kuamini kwa kuuona mwenendo wenu. Haitakuwa lazima kwenu kusema neno,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kadhalika enyi wake, watiini waume zenu, ili kama kunao wasioamini lile neno, wapate kuvutwa na mwenendo wa wake zao pasipo neno,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Vivyo hivyo, enyi wake mnapaswa kuwa radhi kuwahudumia waume zenu. Ili hata wale waliokataa kuyapokea mafundisho ya Mungu washawishike na kuamini kutokana na jinsi mnavyoishi. Hivyo hamtahitaji kusema chochote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nanyi wake, jiwekeni chini ya mamlaka ya waume zenu, ili kama wako waume wowote wasioamini neno la Mungu, wapate kuamini kwa kuuona mwenendo wenu. Haitakuwa lazima kwenu kusema neno,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nanyi wake, jiwekeni chini ya mamlaka ya waume zenu, ili kama wako waume wowote wasioamini neno la Mungu, wapate kuamini kwa kuuona mwenendo wenu. Haitakuwa lazima kwenu kusema neno,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kadhalika enyi wake, watiini waume zenu, ili kama wako wasioamini lile neno, wapate kuvutwa na mwenendo wa wake zao pasipo neno,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kadhalika enyi wake, watiini waume zenu, ili kama kunao wasioamini lile neno, wapate kuvutwa na mwenendo wa wake zao pasipo neno,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nanyi wake, jiwekeni chini ya mamlaka ya waume zenu, ili kama wako waume wowote wasioamini neno la Mungu, wapate kuamini kwa kuuona mwenendo wenu. Haitakuwa lazima kwenu kusema neno,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vivyo hivyo nanyi wake sharti mwatii waume wenu! Maana kama wako wasiolitii Neno, watatekwa kwa mwenendo wa wake zao pasipo kuambiwa maneno,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninyi wake, muwatii waume wenu, kusudi kukiwa wamoja kati yao wasioamini neno la Mungu, mupate kuwavuta kwa kulisadiki kwa mwenendo wenu muzuri pasipo kuwaambia neno.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
KADHALIKA ninyi wake, watumikieni waume o zenu; kusudi, ikiwa wako waume wasioliamini Neno, kwa mwenendo wa wake zao, pasipo Neno lile, wavutwe;