1 Peter 3:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
lakini fanyeni hivyo kwa upole na heshima. Muwe na dhamiri njema, kusudi mnapotukanwa, wale wanaosema ubaya juu ya mwenendo wenu mwema kama Wakristo, waone aibu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
mkizitunza dhamiri zenu ziwe safi, ili wale wasemao mabaya dhidi ya mwenendo wenu mzuri katika Al-Masihi waaibike kwa ajili ya masingizio yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nanyi mwe na dhamiri njema, ili katika neno lile mnalosingiziwa, watahayarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini wajibuni kwa upole na heshima kwa ajili ya Mungu, mkizitunza dhamiri zenu mbele zake. Ndipo watu watakapoona namna njema mnayoishi kama wafuasi wa Kristo. Na wataaibika kwa kuwanenea mabaya.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
lakini fanyeni hivyo kwa upole na heshima. Muwe na dhamiri njema, kusudi mnapotukanwa, wale wanaosema ubaya juu ya mwenendo wenu mwema kama Wakristo, waone aibu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
lakini fanyeni hivyo kwa upole na heshima. Muwe na dhamiri njema, kusudi mnapotukanwa, wale wanaosema ubaya juu ya mwenendo wenu mwema kama Wakristo, waone aibu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
mkizitunza dhamiri zenu ziwe safi, ili wale wasemao mabaya dhidi ya mwenendo wenu mzuri katika Kristo, waaibike kwa ajili ya masingizio yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
mkizitunza dhamiri zenu ziwe safi, ili wale wasemao mabaya dhidi ya mwenendo wenu mzuri katika Al-Masihi waaibike kwa ajili ya masingizio yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nanyi muwe na dhamiri njema, ili katika neno lile mnalosingiziwa, watahayarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
lakini fanyeni hivyo kwa upole na heshima. Muwe na dhamiri njema, kusudi mnapotukanwa, wale wanaosema ubaya juu ya mwenendo wenu mwema kama Wakristo, waone aibu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mioyo yenu sharti ijulike kuwa miema! Hivyo wenye kuwasengenya kwamba: M waovu, wataingiwa na soni kwa ajili ya mwenendo wenu, ukiwa mzuri kwa nguvu ya Kristo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nanyi mwe na dhamiri njema, ili katika neno lile mnalosingiziwa, watahayarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
mukiwa na zamiri safi, hata wale wanaowasingizia na kuwatukana juu ya mwenendo wenu muzuri katika ushirika wenu na Kristo, wapate haya.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
mkiwa na dhamiri njema, illi katika neno lile mnalosingiziwa kwamba m watenda mabaya, wataha yarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo.