1 Peter 3:18 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa maana Kristo mwenyewe alikufa kwa ajili ya dhambi zenu; alikufa mara moja tu na ikatosha, mtu mwema kwa ajili ya waovu, ili awapeleke nyinyi kwa Mungu. Aliuawa kimwili lakini akafanywa hai kiroho;
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa Al-Masihi naye aliteswa mara moja tu kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili ya wasio haki, ili awalete ninyi kwa Mungu. Mwili wake ukauawa, lakini akafanywa hai katika Roho wa Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kristo mwenyewe aliteseka alipokufa kwa ajili yenu, na kwa kifo hicho kimoja alilipa fidia kwa ajili ya dhambi. Hakuwa na hatia, lakini alikufa kwa ajili ya watu waliokuwa na hatia. Alifanya hivyo ili awalete ninyi nyote kwa Mungu. Kama mwanadamu, aliuawa, lakini uhai wake ulifanywa hai na Roho.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa maana Kristo mwenyewe alikufa kwa ajili ya dhambi zenu; alikufa mara moja tu na ikatosha, mtu mwema kwa ajili ya waovu, ili awapeleke ninyi kwa Mungu. Aliuawa kimwili lakini akafanywa hai kiroho;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa maana Kristo mwenyewe alikufa kwa ajili ya dhambi zenu; alikufa mara moja tu na ikatosha, mtu mwema kwa ajili ya waovu, ili awapeleke nyinyi kwa Mungu. Aliuawa kimwili lakini akafanywa hai kiroho;
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa Kristo naye aliteswa mara moja tu, mwenye haki kwa ajili ya wasio na haki, ili awalete ninyi kwa Mungu. Mwili wake ukauawa, lakini akafanywa hai katika Roho,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa Al-Masihi naye aliteswa mara moja tu kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili ya wasio haki, ili awalete ninyi kwa Mungu. Mwili wake ukauawa, lakini akafanywa hai katika Roho.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; akauawa kimwili, lakini akahuishwa kiroho,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa maana Kristo mwenyewe alikufa kwa ajili ya dhambi zenu; alikufa mara moja tu na ikatosha, mtu mwema kwa ajili ya waovu, ili awapeleke nyinyi kwa Mungu. Aliuawa kimwili lakini akafanywa hai kiroho;
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani naye Kristo alikufa mara moja kwa ajili ya makosa yetu; yeye aliyekuwa mwongofu alikufa kwa ajili yetu tulio wapotovu, atupeleke kwake Mungu. Aliuawa kimwili, lakini alirudishwa uzimani Kiroho.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kufuatana na hiyo, Kristo naye alikufa mara moja tu kwa sababu ya zambi zenu. Yeye alikuwa mwenye haki kwa ajili ya waovu, kusudi awaonyeshe ninyi njia ya kumufuata Mungu. Aliuawa kimwili, lakini kwa uwezo wa Roho Mutakatifu alipata tena uzima.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana Kristo nae aliteswa marra moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio baki, illi atulete kwa Mungu; mwili wake akifishwa, bali roho yake akihuishwa.