1 Peter 3:20 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hao ndio wale waliokataa kumtii Mungu alipowangoja kwa saburi wakati Noa alipokuwa anatayarisha ile safina. Ndani ya chombo hicho ni watu wachache tu, yaani watu wanane, waliookolewa katika maji,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
roho ambazo zamani hazikutii, wakati ule uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja katika siku za Nuhu, wakati wa kujenga safina, ambamo watu wachache tu, yaani watu wanane, waliokolewa ili wasiangamie kwa gharika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hizo ndizo roho zilizokataa kumtii Mungu hapo zamani wakati wa Nuhu. Mungu alisubiri kwa uvumilivu Nuhu alipokuwa anaunda safina. Na watu wachache tu, yaani wanane kwa jumla ndiyo walioingia katika safina na kuokolewa kwa kuvushwa salama katika gharika hiyo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hao ndio wale waliokataa kumtii Mungu alipowangoja kwa saburi wakati Noa alipokuwa anatayarisha ile safina. Ndani ya chombo hicho ni watu wachache tu, yaani watu wanane, waliookolewa majini,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hao ndio wale waliokataa kumtii Mungu alipowangoja kwa saburi wakati Noa alipokuwa anatayarisha ile safina. Ndani ya chombo hicho ni watu wachache tu, yaani watu wanane, waliookolewa katika maji,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Roho hizo ambazo zamani hazikutii, wakati ule uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja katika siku za Noa, wakati wa kujenga safina, ambako watu wachache tu, yaani, watu wanane waliokolewa wasiangamie kwa gharika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
roho hizo ambazo zamani hazikutii, wakati ule uvumilivu wa Mwenyezi Mungu ulipokuwa ukingoja katika siku za Nuhu, wakati wa kujenga safina, ambamo watu wachache tu, yaani watu wanane, waliokolewa ili wasiangamie kwa gharika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
watu wasiotii hapo zamani, wakati Mungu alipowavumilia kwa subira, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hao ndio wale waliokataa kumtii Mungu alipowangoja kwa saburi wakati Noa alipokuwa anatayarisha ile safina. Ndani ya chombo hicho ni watu wachache tu, yaani watu wanane, waliookolewa katika maji,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wale waliokataa kutii kale, Mungu alipowangoja na kuwavumilia siku zile za Noa, kile chombo kikubwa kilipotengenezwa; lakini miongoni mwao wakaokoka wachache, watu wanane tu katika kondo ile ya maji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Roho zile ni za watu walioasi Mungu zamani za kale alipowavumilia katika siku Noa alipotengeneza chombo kikubwa. Ni watu wanane tu ndio waliingia ndani ya chombo na kuokolewa katika maji.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
akawakhubiri watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ndani yake watu wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji.