1 Peter 3:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sara kwa mfano alimtii Abrahamu na kumwita yeye bwana. Nyinyi mmekuwa sasa binti zake kama mkitenda mema bila kuogopa tisho lolote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kama Sara alivyomtii mumewe Ibrahimu, hata akamwita bwana. Ninyi ni watoto wa Sara mkitenda yaliyo mema, bila kuogopa jambo lolote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yo yote.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninazungumza juu ya wanawake kama Sara aliyemtii Ibrahimu, mume wake na kumwita bwana wake. Na ninyi wanawake ni watoto wa kweli wa Sara ikiwa daima mnafanya yale yaliyo sahihi pasipokuwa na hofu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Sara kwa mfano alimtii Abrahamu na kumwita yeye bwana. Ninyi mmekuwa sasa binti zake kama mkitenda mema bila kuogopa tisho lolote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sara kwa mfano alimtii Abrahamu na kumwita yeye bwana. Nyinyi mmekuwa sasa binti zake kama mkitenda mema bila kuogopa tisho lolote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kama Sara alivyomtii mumewe Abrahamu, akamwita bwana. Ninyi ni watoto wa Sara kama mkitenda yaliyo mema na bila kuogopa jambo lo lote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kama Sara alivyomtii mumewe Ibrahimu, hata akamwita bwana. Ninyi ni watoto wa Sara kama mkitenda yaliyo mema, bila kuogopa jambo lolote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kama vile Sara alivyomtii Abrahamu, akamwita bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, pasipo kutishwa na hofu yoyote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sara kwa mfano alimtii Abrahamu na kumwita yeye bwana. Nyinyi mmekuwa sasa binti zake kama mkitenda mema bila kuogopa tisho lolote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kama Sara alivyomtii Aburahamu akimwita bwana. Nanyi wanawake, mnakuwa watoto wake mkitenda mema pasipo kuogopa vituko vyo vyote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yo yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni vile Sara alimutii Abrahamu, akimwita “Bwana.” Ninyi ni wabinti zake kama mukifanya mema pasipo kuogopa kitisho chochote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; ninyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala kushitushwa kwa khofu yo yote.