1 Peter 4:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Anayesema kitu, maneno yake na yawe kama maneno ya Mungu; anayetumikia anapaswa kutumikia kwa nguvu anayojaliwa na Mungu, ili katika mambo yote, Mungu atukuzwe kwa njia ya Yesu Kristo ambaye utukufu na nguvu ni vyake milele na milele! Amina.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeyote asemaye hana budi kusema kama mtu asemaye maneno ya Mungu mwenyewe. Yeyote anayehudumu hana budi kuhudumu kwa nguvu zile anazopewa na Mungu, ili Mungu apate kutukuzwa katika mambo yote kupitia kwa Isa Al-Masihi. Utukufu na uweza una yeye milele na milele. Amen.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ikiwa kipawa chako ni kuhubiri, maneno yako yawe kama yanayotoka kwa Mungu. Ikiwa kipawa chako ni kuhudumu, unatakiwa kuhudumu kwa nguvu anazokupa Mungu. Ndipo Mungu atakaposifiwa kwa kila jambo katika Yesu Kristo. Uwezo na utukufu ni wake milele na milele. Amina.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Anayesema kitu, maneno yake na yawe kama maneno ya Mungu; anayetumika anapaswa kutumikia kwa nguvu anayojaliwa na Mungu, ili katika mambo yote, Mungu atukuzwe kwa njia ya Yesu Kristo, ambaye utukufu na nguvu ni vyake milele na milele! Amina.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Anayesema kitu, maneno yake na yawe kama maneno ya Mungu; anayetumikia anapaswa kutumikia kwa nguvu anayojaliwa na Mungu, ili katika mambo yote, Mungu atukuzwe kwa njia ya Yesu Kristo ambaye utukufu na nguvu ni vyake milele na milele! Amina.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ye yote asemaye hana budi kusema kama mtu asemaye maneno ya Mungu mwenyewe. Ye yote ahudumuye hana budi kuhudumu kwa nguvu zile apewazo na Mungu, ili Mungu apate kutukuzwa katika mambo yote kwa njia ya Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye milele na milele. Amen.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yeyote asemaye hana budi kusema kama mtu asemaye maneno ya Mungu mwenyewe. Yeyote ahudumuye hana budi kuhudumu kwa nguvu zile anazopewa na Mwenyezi Mungu, ili Mungu apate kutukuzwa katika mambo yote kwa njia ya Isa Al-Masihi. Utukufu na uweza una yeye milele na milele. Amen.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtu akisema, na aseme kama asemaye maneno halisi ya Mungu; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Anayesema kitu, maneno yake na yawe kama maneno ya Mungu; anayetumikia anapaswa kutumikia kwa nguvu anayojaliwa na Mungu, ili katika mambo yote, Mungu atukuzwe kwa njia ya Yesu Kristo ambaye utukufu na nguvu ni vyake milele na milele! Amina.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtu akisema na ayaseme, kama ni kusema maneno ya Mungu! Mtu akitumika na atumike kwa kuwa mtu aliyepewa nguvu na Mungu kwamba: Katika mambo yote Mungu atukuzwe kwa ajili ya Yesu Kristo! Wake yeye ni utukufu na uwezo kale na kale pasipo mwisho! Amin.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule anayehubiri, anapaswa kutoa ujumbe wa Mungu. Na yule anayetumika, atumike kwa kadiri ya nguvu alizopewa na Mungu, kusudi Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa njia ya Yesu Kristo anayekuwa mwenye utukufu na uwezo kwa milele na milele. Amina.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akikhudumu, na akhudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; illi Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo; utukufu na uweza u kwake hatta milele na milele. Amin.