1 Peter 4:15 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Asiwepo mtu yeyote miongoni mwenu ambaye anapaswa kuteseka kwa sababu ni mwuaji, mwizi, mhalifu au mwovu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini asiwepo mtu yeyote miongoni mwenu anayeteswa kwa kuwa ni muuaji, au mwizi, au mhalifu wa aina yoyote, au anayejishughulisha na mambo ya watu wengine.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana mtu wa kwenu asiteswe kama mwuaji, au mwivi, au mtenda mabaya, au kama mtu ajishughulishaye na mambo ya watu wengine.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mnaweza kupata mateso; lakini msiteseke kwa sababu mmeua, mmeiba, mmesababisha ghasia, au mmejaribu kutawala maisha ya watu wengine.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Asiwepo mtu yeyote miongoni mwenu ambaye anapaswa kuteseka kwa sababu ni muuaji, mwizi, mhalifu au mwovu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Asiwepo mtu yeyote miongoni mwenu ambaye anapaswa kuteseka kwa sababu ni mwuaji, mwizi, mhalifu au mwovu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini asiwepo mtu ye yote miongoni mwenu anayeteswa kwa kuwa ni mwuaji, au mwivi, au mhalifu au anayejishughulisha na mambo ya watu wengine, ili kuwagombanisha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini asiwepo mtu yeyote miongoni mwenu anayeteswa kwa kuwa ni muuaji, au mwizi, au mhalifu wa aina yoyote, au anayejishughulisha na mambo ya watu wengine.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini pasiwe na hata mmoja wenu atakayeteseka kwa kuwa mwuaji, mwizi, mhalifu au hata mfitini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Asiwepo mtu yeyote miongoni mwenu ambaye anapaswa kuteseka kwa sababu ni mwuaji, mwizi, mhalifu au mwovu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kwenu asioneke ateswaye kwa kuwa mwuaji au mwizi au mtenda maovu au mkaguzi wa mambo yasiyo yake!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana mtu wa kwenu asiteswe kama mwuaji, au mwivi, au mtenda mabaya, au kama mtu ajishughulishaye na mambo ya watu wengine.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kati yenu kusikuwe hata mutu mumoja anayeteswa kwa sababu yeye ni mwuaji, mwizi, mutenda mabaya au mwenye kujiingiza katika mambo ya watu wengine.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana mtu wa kwenu asiteswe kama muuaji, au mwizi, au mtenda mabaya, au kama mtu ajishughulishae na mambo ya watu wengine.