1 Peter 4:16 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kama mtu akiteseka kwa sababu ni Mkristo, basi, asione aibu, bali amtukuze Mungu, kwa sababu mtu huyo anaitwa kwa jina la Kristo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ukiteseka kwa kuwa mfuasi wa Al-Masihi, usihesabu jambo hilo kuwa ni aibu, bali mtukuze Mungu kwa sababu umeitwa kwa jina hilo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini endapo utateswa kwa kuwa ni “Mkristo” basi usione haya. Bali umshukuru Mungu kwa kuwa unalibeba jina hilo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini kama mtu akiteseka kwa sababu ni Mkristo, basi asione aibu, bali amtukuze Mungu, kwa sababu mtu huyo anaitwa kwa jina la Kristo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kama mtu akiteseka kwa sababu ni Mkristo, basi, asione aibu, bali amtukuze Mungu, kwa sababu mtu huyo anaitwa kwa jina la Kristo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kama mtu ye yote akiteseka kwa kuwa ni mkristo, asihesabu jambo hilo kuwa ni aibu, bali amtukuze Mungu kwa sababu ameitwa kwa jina hilo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kama ukiteseka kwa kuwa mfuasi wa Al-Masihi, usihesabu jambo hilo kuwa ni aibu, bali mtukuze Mungu kwa sababu umeitwa kwa jina hilo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini ikiwa mtu yeyote miongoni mwenu anateseka kwa sababu ni Mkristo, asione haya, bali amtukuze Mungu maana ana jina hili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kama mtu akiteseka kwa sababu ni Mkristo, basi, asione aibu, bali amtukuze Mungu, kwa sababu mtu huyo anaitwa kwa jina la Kristo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mtu akiteseka kwa kuwa Mkristo, asione soni, ila amtukuze Mungu kwa kuwamo katika Jina hili!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini mutu akiteswa kwa sababu yeye ni mukristo, asione haya, lakini atukuze Mungu kwa kuwa anaitwa kwa jina lile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Illakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hili.