1 Peter 4:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati wa hukumu umefika, na hukumu hiyo inaanza na watu wake Mungu mwenyewe. Ikiwa hukumu hiyo inaanzia kwetu sisi, basi, mwisho wake utakuwa namna gani kwa wale wasioamini Habari Njema ya Mungu?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana wakati umewadia wa hukumu kuanzia katika nyumba ya Mungu. Basi ikianzia kwetu sisi, mwisho wa hao wasiotii Injili ya Mungu utakuwaje?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakati wa kuanza hukumu umewadia. Hukumu hiyo itaanza na familia ya Mungu. Ikiwa itaanzia kwetu, nini kitawatokea wale wasioikubali Habari Njema ya Mungu?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakati wa hukumu umefika, na hukumu hiyo inaanza na watu wake Mungu mwenyewe. Ikiwa hukumu hiyo inaanzia kwetu sisi, basi mwisho wake utakuwa namna gani kwa wale wasioamini Habari Njema ya Mungu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati wa hukumu umefika, na hukumu hiyo inaanza na watu wake Mungu mwenyewe. Ikiwa hukumu hiyo inaanzia kwetu sisi, basi, mwisho wake utakuwa namna gani kwa wale wasioamini Habari Njema ya Mungu?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana wakati umewadia wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu. Basi kama ikianza kwetu sisi, mwisho wa hao wasiotii Injili ya Mungu utakuwaje?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana wakati umewadia wa hukumu kuanzia katika nyumba ya Mwenyezi Mungu. Basi kama ikianzia kwetu sisi, mwisho wa hao wasiotii Injili ya Mungu utakuwaje?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii Injili ya Mungu utakuwaje?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati wa hukumu umefika, na hukumu hiyo inaanza na watu wake Mungu mwenyewe. Ikiwa hukumu hiyo inaanzia kwetu sisi, basi, mwisho wake utakuwa namna gani kwa wale wasioamini Habari Njema ya Mungu?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani siku zimetimia, hukumu ianze kwao walio wa Nyumba ya Mungu. Basi, ikianza kwetu itakuwaje mwishoni kwao waliokataa kutii Utume mwema wa Mungu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati wa hukumu unakaribia. Na hukumu itaanza na watu wa Mungu. Na kama hukumu inaanzia kwetu sisi, basi mwisho wake utakuwa namna gani kwa wale wasiotii Habari Njema ya Mungu?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana wakati umefika hukumu ianzie nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu, nini mwisho wao wasioitu Injili ya Mungu?