1 Peter 4:2 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tangu sasa, basi, maisha yaliyowabakia kuishi hapa duniani yanapaswa kuongozwa na matakwa ya Mungu, sio na tamaa za kibinadamu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hivyo, haishi maisha yake yaliyobaki hapa duniani ili kutimiza tamaa mbaya za wanadamu, bali anaishi ili kutimiza mapenzi ya Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Jiimarishe wenyewe ili mweze kuishi maisha yenu yaliyosalia hapa duniani kwa kutenda yale anayotaka Mungu, siyo maovu ambayo watu wanataka kufanya.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tangu sasa, basi, maisha yaliowabakia kuishi hapa duniani yanapaswa kuongozwa na matakwa ya Mungu, si na tamaa za kibinadamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tangu sasa, basi, maisha yaliyowabakia kuishi hapa duniani yanapaswa kuongozwa na matakwa ya Mungu, sio na tamaa za kibinadamu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Matokeo yake, maisha yake yaliyobaki ya kuishi hapa duniani, haishi tena kwa kufuata tamaa mbaya za wanadamu, bali anaishi kwa kufuata mapenzi ya Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hivyo, haishi maisha yake yaliyobaki ya kuishi hapa duniani kwa tamaa mbaya za wanadamu, bali anaishi kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tangu sasa, basi, maisha yaliyowabakia kuishi hapa duniani yanapaswa kuongozwa na matakwa ya Mungu, sio na tamaa za kibinadamu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
nazo siku zake zilizosalia za kuwapo mwilini hatazimaliza na kuzifuata tamaa za watu, ila atafanya, Mungu ayatakayo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa, musiishi tena kufuatana na tamaa za kimutu, lakini muishi kufuatana na mapenzi ya Mungu kwa muda unaowabakilia kwa kukaa katika dunia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kuanzia sasa tusiendelee kuishi katika tamaa za wana Adamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wetu wa kukaa hapa duniani uliobakia.