1 Peter 4:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwisho wa vitu vyote umekaribia. Kwa hiyo mnapaswa kuwa na utaratibu na kukesha ili muweze kusali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwisho wa mambo yote umekaribia. Kwa hiyo kuweni na tahadhari, mkiwa na akili tulivu na kujidhibiti, mkikesha katika kuomba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika sala.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakati wa kila kitu kufikia mwisho wake umekaribia. Hivyo iweni waangalifu katika akili zenu na mjizuie kwa kila jambo. Hii itawasaidia katika maombi yenu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mwisho wa vitu vyote umekaribia. Kwa hiyo mnapaswa kuwa na utaratibu na nidhamu, ili mweze kusali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwisho wa vitu vyote umekaribia. Kwa hiyo mnapaswa kuwa na utaratibu na kukesha ili muweze kusali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwisho wa mambo yote umekaribia. Kwa hiyo iweni na akili pia mwe na kiasi mkikesha katika kuomba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwisho wa mambo yote umekaribia. Kwa hiyo kuweni na akili tulivu na kiasi, mkikesha katika kuomba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika sala.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwisho wa vitu vyote umekaribia. Kwa hiyo mnapaswa kuwa na utaratibu na kukesha ili muweze kusali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwisho wa vitu vyote uko karibu. Kwa hiyo mjiangalie, mlevuke, mpate kuomba!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika sala.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwisho wa vitu vyote unakaribia kutimia. Kwa hiyo mukuwe wenye akili na waangalifu, kusudi mukuwe na uwezo wa kuomba.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mwisho wa mamho yote umekaribia; bassi, mwe na akili, mkakeshe katika sala: