1 Peter 5:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi mzee miongoni mwenu wazee wenzangu, mimi ambaye nilishuhudia mateso ya Kristo na kushiriki ule utukufu utakaofunuliwa, nawasihini
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa wazee walio miongoni mwenu, nawasihi mimi nikiwa mzee mwenzenu, shahidi wa mateso ya Al-Masihi, na mshiriki katika utukufu utakaofunuliwa:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawasihi wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadaye;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sasa nina jambo la kuwaambia wazee walio katika kundi lenu. Mimi pia ni mzee nami mwenyewe nimeyaona mateso ya Kristo. Na nitashiriki katika utukufu utakaodhihirishwa kwetu. Hivyo ninawasihi,
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
wazee! Mimi niliye mzee ninalo ombi moja kwenu wazee wenzangu. Mimi mwenyewe nilishuhudia kwa macho yangu mateso ya Kristo na natumaini kuushiriki ule utukufu utakaofunuliwa. Mimi nawaombeni
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi mzee miongoni mwenu wazee wenzangu, mimi ambaye nilishuhudia mateso ya Kristo na kushiriki ule utukufu utakaofunuliwa, nawasihini
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa wazee waliomo miongoni mwenu, nawasihi mimi nikiwa mzee mwenzenu, shahidi wa mateso ya Kristo na mshiriki katika utukufu utakaofunuliwa,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa wazee waliomo miongoni mwenu, nawasihi mimi nikiwa mzee mwenzenu, shahidi wa mateso ya Al-Masihi, na mshiriki katika utukufu utakaofunuliwa:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawasihi wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadaye;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi mzee miongoni mwenu wazee wenzangu, mimi ambaye nilishuhudia mateso ya Kristo na kushiriki ule utukufu utakaofunuliwa, nawasihini
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wazee walioko kwenu nawaonya mimi niliye mzee mwenzao na shahidi wa mateso yake Kristo, nitakayekuwa mwenziwe hata katika utukufu utakaofunuliwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawasihi wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadaye;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninawaonya wazee wa kanisa wanaokuwa kati yenu. Mimi vilevile ni muzee mwenzenu, nami ni mushuhuda wa mateso ya Kristo na zaidi ya hii nitashiriki katika utukufu ule utakaotokea.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
NAWASIHI wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadae;