1 Peter 5:10 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini mkisha teseka muda mfupi, Mungu aliye asili ya neema yote na ambaye anawaiteni kuushiriki utukufu wake wa milele katika kuungana na Kristo, yeye mwenyewe atawakamilisheni na kuwapeni uthabiti, nguvu na msingi imara.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nanyi baada ya kuteswa kwa kitambo kidogo, Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele ndani ya Al-Masihi, yeye mwenyewe atawarejesha na kuwatia nguvu, akiwaimarisha na kuwathibitisha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, na kuwathibitisha, na kuwatia nguvu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndiyo, mtateseka kwa muda mfupi. Lakini baada ya hapo, Mungu ataweka kila kitu sawa. Atawatia nguvu, atawasaidia na kuwashika msianguke. Yeye ni Mungu ndiye chanzo cha neema yote. Aliwachagua mshiriki katika utukufu wake ndani ya Kristo. Utukufu huo utadumu milele.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini mkisha teseka muda mfupi, Mungu aliye asili ya neema yote na ambaye anawaiteni muushiriki utukufu wake wa milele katika kuungana na Kristo, yeye mwenyewe atawakamilisheni na kuwapeni uthabiti, nguvu na msingi imara.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini mkisha teseka muda mfupi, Mungu aliye asili ya neema yote na ambaye anawaiteni kuushiriki utukufu wake wa milele katika kuungana na Kristo, yeye mwenyewe atawakamilisheni na kuwapeni uthabiti, nguvu na msingi imara.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nanyi mkiisha kuteswa kwa kitambo kidogo, Mungu wa neema yote aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele ndani ya Kristo, yeye mwenyewe atawatengeneza upya, atawasaidia, atawatia nguvu na kuwathibitisha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nanyi mkiisha kuteswa kwa kitambo kidogo, Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele ndani ya Al-Masihi, yeye mwenyewe atawarejesha na kuwatia nguvu, akiwaimarisha na kuwathibitisha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawaimarisha, atawathibitisha, atawatia nguvu na kuwapa msingi imara.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini mkisha teseka muda mfupi, Mungu aliye asili ya neema yote na ambaye anawaiteni kuushiriki utukufu wake wa milele katika kuungana na Kristo, yeye mwenyewe atawakamilisheni na kuwapeni uthabiti, nguvu na msingi imara.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Mungu mwenye mema yote ya kuwagawia, aliyewaitia nanyi utukufu wake wa kale na kale uliomo katika Kristo, atawalinganya mwenyewe, mkiteseka kidogo, na kuwapa uwezo na nguvu na msingi mgumu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, na kuwathibitisha, na kuwatia nguvu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini mukisha kuteswa kwa muda kidogo, Mungu mwenye neema yote aliyewaita kusudi mupate kushiriki naye katika utukufu wake wa milele katika kuungana kwenu na Kristo, yeye mwenyewe atawakamilisha. Atawatia nguvu na kuwasimamisha imara kabisa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, atawathubutisha, atawatia nguvu.