1 Peter 5:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nimewaandikieni barua hii fupi kwa msaada wa Silwano, ndugu ambaye namjua na kumwamini. Nataka kuwapeni moyo na kushuhudia kwamba jambo hili ni neema ya Mungu kweli. Kaeni imara katika neema hiyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa msaada wa Silvano, ninayemhesabu kuwa ndugu mwaminifu, nimewaandikia waraka huu mfupi ili kuwatia moyo, na kushuhudia kwamba hii ni neema halisi ya Mungu. Simameni imara katika neema hiyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa mkono wa Silwano, ndugu mwaminifu kama nionavyo, nimewaandikia kwa maneno machache, kuonya na kushuhudia ya kuwa hii ndiyo neema ya kweli ya Mungu. Simameni imara katika hiyo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sila ataileta barua hii kwenu. Nafahamu kwamba ni ndugu mwaminifu katika familia ya Mungu. Niliandika barua hii fupi kuwatia moyo na kuwaambia kuwa hii ni neema ya kweli ya Mungu. Simameni imara katika neema hiyo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nimewaandikieni barua hii fupi kwa msaada wa Silwano, ndugu ambaye namjua na kumwamini. Nataka kuwapeni moyo na kushuhudia kwamba jambo hili ni neema ya Mungu kweli. Kaeni imara katika neema hiyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nimewaandikieni barua hii fupi kwa msaada wa Silwano, ndugu ambaye namjua na kumwamini. Nataka kuwapeni moyo na kushuhudia kwamba jambo hili ni neema ya Mungu kweli. Kaeni imara katika neema hiyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa msaada wa Silvano, yeye ambaye ninamhesabu kuwa ndugu mwaminifu, nimewaandikia waraka huu mfupi ili kuwatia moyo na kushuhudia kwamba hii ni neema halisi ya Mungu. Simameni imara katika neema hiyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa msaada wa Silvano, ambaye ninamhesabu kuwa ndugu mwaminifu, nimewaandikia waraka huu mfupi ili kuwatia moyo, na kushuhudia kwamba hii ni neema halisi ya Mwenyezi Mungu. Simameni imara katika neema hiyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa mkono wa Silwano, ndugu mwaminifu kama nijuavyo, nimewaandikia kwa maneno machache, kuonya na kushuhudia ya kuwa hii ndiyo neema ya kweli ya Mungu. Simameni imara katika hiyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nimewaandikieni barua hii fupi kwa msaada wa Silwano, ndugu ambaye namjua na kumwamini. Nataka kuwapeni moyo na kushuhudia kwamba jambo hili ni neema ya Mungu kweli. Kaeni imara katika neema hiyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nimewaandikia kidogo kwa mkono wa ndugu Silwano, ninayemwona kuwa mwelekevu. Nimewaonya na kuwashuhudia kwamba: Mmegawiwa mema ya Mungu yaliyo ya kweli. Nayo yakalieni!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa mkono wa Silwano, ndugu mwaminifu kama nionavyo, nimewaandikia kwa maneno machache, kuonya na kushuhudia ya kuwa hii ndiyo neema ya kweli ya Mungu. Simameni imara katika hiyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nimewaandikia barua hii fupi nikisaidiwa na Sila, ninayemujua kuwa ndugu mwaminifu. Ninataka kuwatia moyo na kushuhudia kwenu kwamba mambo hayo yanayoelekea neema ya Mungu ni ya kweli; nanyi musikose kushikamana nayo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa mkono wa Silwano, ndugu mwaminifu kama nionavyo, nimewaandikieni kwa maneno machache, nikionya na kushuhudia ya kuwa hii ndiyo neema ya kweli va Mungu. Simameni imara katika hiyo.