1 Peter 5:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jumuiya ya wenzenu walioteuliwa na Mungu hapa Babuloni wanawasalimuni. Vilevile mwanangu Marko anawasalimuni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kundi la waumini lililoko Babeli, lililochaguliwa pamoja nanyi, wanawasalimu; vivyo hivyo mwanangu Marko anawasalimu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwenzenu mteule hapa Babeli awasalimu, na Marko mwanangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kanisa lililoko Babeli linatuma salamu kwenu. Wameteuliwa kama ninyi. Marko, ambaye ni kama mwanangu kwangu katika Kristo, anawasalimu pia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Jumuiya ya wenzenu walioteuliwa na Mungu hapa Babuloni wanawasalimuni. Vilevile mwanangu Marko anawasalimuni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jumuiya ya wenzenu walioteuliwa na Mungu hapa Babuloni wanawasalimuni. Vilevile mwanangu Marko anawasalimuni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kanisa lililoko Babeli, lililochaguliwa pamoja nanyi, wanawasalimu; vivyo hivyo mwanangu Marko anawasalimu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kundi la waumini lililoko Babeli, lililochaguliwa pamoja nanyi, wanawasalimu; vivyo hivyo mwanangu Marko anawasalimu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwenzenu mteule hapa Babeli awasalimu, na Marko mwanangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jumuiya ya wenzenu walioteuliwa na Mungu hapa Babuloni wanawasalimuni. Vilevile mwanangu Marko anawasalimuni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wateule waliomo humu Babiloni pamoja nasi wanawasalimu, hata mwanangu Marko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwenzenu mteule hapa Babeli awasalimu, na Marko mwanangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kanisa linalokuwa katika Babeli, lililochaguliwa na Mungu kama vile ninyi, linawasalimia. Vilevile Marko, mwana wangu katika imani, anawasalimia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bibi mteule, mwenzi wenu aliye katika Babeli, awasalimu, na Marko mwanangu.