1 Peter 5:2 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
mlichunge lile kundi la Mungu mlilokabidhiwa; mlitunze si kwa kulazimika, bali kwa hiari kama atakavyo Mungu. Fanyeni kazi hiyo si kwa tamaa ya fedha, bali kwa moyo wenu wote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
lichungeni kundi la Mungu mlilokabidhiwa, mkitumika kama waangalizi, si kwa kulazimishwa bali kwa hiari, kama Mungu anavyowataka mwe; si kwa tamaa ya fedha, bali mlio na bidii katika kutumika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
mlitunze kundi la watu mnalowajibika kwalo. Ni kundi lake Mungu. Basi lichungeni kwa moyo wa kupenda na si kwa kulazimishwa. Hivi ndivyo Mungu anavyotaka. Fanyeni hivyo kwa sababu mnafurahi kutumika, na si kwa sababu mnataka pesa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
mlichunge lile kundi la Mungu mlilokabidhiwa, mlitunze si kwa kulazimika, bali kwa hiari kama atakavyo Mungu. Fanyeni kazi hiyo si kwa tamaa ya fedha, bali kwa moyo wenu wote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
mlichunge lile kundi la Mungu mlilokabidhiwa; mlitunze si kwa kulazimika, bali kwa hiari kama atakavyo Mungu. Fanyeni kazi hiyo si kwa tamaa ya fedha, bali kwa moyo wenu wote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
lichungeni kundi la Mungu mlilokabidhiwa, mkitumika kama waangalizi, si kwa kulazimishwa bali kwa hiari, kama Mungu anavyowataka mwe, si kwa tamaa ya fedha, bali mlio na bidii katika kutumika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
lichungeni kundi la Mwenyezi Mungu mlilokabidhiwa, mkitumika kama waangalizi, si kwa kulazimishwa bali kwa hiari, kama Mungu anavyowataka mwe; si kwa tamaa ya fedha, bali mlio na bidii katika kutumika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
mlichunge lile kundi la Mungu mlilokabidhiwa; mlitunze si kwa kulazimika, bali kwa hiari kama atakavyo Mungu. Fanyeni kazi hiyo si kwa tamaa ya fedha, bali kwa moyo wenu wote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nawaonya kwamba: Lichungeni kundi la Mungu lililoko kwenu, si kwa shuruti, ila kwa kuyapenda wenyewe, Mungu ayatakayo, wala si kwa kufuata machumo mabaya, ila kwa mioyo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninawaonya, muchunge lile kundi Mungu alilowapatia, si kwa kulazimishwa, lakini kwa mapenzi yenu sawa vile Mungu anavyotaka. Musitumike kwa ajili ya tamaa mbaya ya mali, lakini kwa kujitoa kwa moyo mwema.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
lichungeni kundi la Kristo lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa khiari; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo;