1 Samuel 1:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hana akasema, “Naomba nami mtumishi wako nipate kibali mbele yako.” Hana akaenda zake, akala chakula na hakuwa na huzuni tena.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hana akasema, “Mtumishi wako na apate kibali machoni pako.” Kisha akaondoka zake na kula chakula, wala uso wake haukuwa na huzuni tena.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye akasema, Mjakazi wako na aone kibali machoni pako. Basi huyo mwanamke akaenda zake, naye akala chakula, wala uso wake haukukunjamana tena.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hana akasema, “Naomba nami mtumishi wako nipate kibali mbele yako.” Hana akaenda zake, akala chakula na hakuwa na huzuni tena.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hana akasema, “Mtumishi wako na apate kibali machoni pako.” Kisha akaondoka zake na kula chakula, wala uso wake haukuwa na huzuni tena.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hana akasema, “Mtumishi wako na apate kibali machoni pako.” Kisha akaondoka zake na kula chakula, wala uso wake haukuwa na huzuni tena.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye akasema, Mjakazi wako na aone kibali machoni pako. Basi huyo mwanamke akaenda zake, naye akala chakula, wala uso wake haukuhuzunika tena.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hana akasema, “Naomba nami mtumishi wako nipate kibali mbele yako.” Hana akaenda zake, akala chakula na hakuwa na huzuni tena.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akasema: Kijakazi wako na ayaone macho yako, yakimtazama kwa upole. Kisha huyo mwanamke akaenda zake, hata kula akala, nao uso wake haukuwa tena kama hapo kwanza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye akasema, Mjakazi wako na aone kibali machoni pako. Basi huyo mwanamke akaenda zake, naye akala chakula, wala uso wake haukukunjamana tena.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hana akasema: “Ninaomba nami mujakazi wako nipate kukubaliwa mbele yako.” Hana akaenda zake, akakula chakula na hakukuwa na huzuni tena.