1 Samuel 1:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kesho yake asubuhi, Elkana na jamaa yake waliamka asubuhi na mapema, na baada ya kumwabudu Mwenyezi-Mungu, walirudi nyumbani Rama. Elkana akalala na mkewe Hana, naye Mwenyezi-Mungu akamkumbuka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kesho yake asubuhi na mapema waliamka wakaabudu mbele za Mwenyezi Mungu na kisha wakarudi nyumbani mwao huko Rama. Elkana akakutana kimwili na mkewe Hana, naye Mwenyezi Mungu akamkumbuka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakaondoka asubuhi na mapema, wakasali mbele za Bwana, kisha wakarejea na kufika nyumbani kwao huko Rama; Elkana akamjua mkewe Hana; naye Bwana akamkumbuka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kesho yake asubuhi, Elkana na jamaa yake waliamka asubuhi na mapema, na baada ya kumwabudu Mwenyezi-Mungu, walirudi nyumbani Rama. Elkana akalala na mkewe Hana, naye Mwenyezi-Mungu akamkumbuka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kesho yake asubuhi na mapema waliamka wakaabudu mbele za BWANA na kisha wakarudi nyumbani kwao huko Rama. Elikana akakutana kimwili na mkewe Hana, naye BWANA akamkumbuka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kesho yake asubuhi na mapema waliamka wakaabudu mbele za bwana na kisha wakarudi nyumbani kwao huko Rama. Elikana akakutana kimwili na mkewe Hana, naye bwana akamkumbuka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakaondoka asubuhi na mapema, wakaomba mbele za BWANA, kisha wakarejea na kufika nyumbani kwao huko Rama; Elkana akamjua mkewe Hana; naye BWANA akamkumbuka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kesho yake asubuhi, Elkana na jamaa yake waliamka asubuhi na mapema, na baada ya kumwabudu Mwenyezi-Mungu, walirudi nyumbani Rama. Elkana akalala na mkewe Hana, naye Mwenyezi-Mungu akamkumbuka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kesho yake wakaamka na mapema, wakaja kumwangukia Bwana, kisha wakarudi kwenda nyumbani kwao huko Rama. Elkana alipomtambua mkewe Hana, Bwana naye akamkumbuka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakaondoka asubuhi na mapema, wakasali mbele za BWANA, kisha wakarejea na kufika nyumbani kwao huko Rama; Elkana akamjua mkewe Hana; naye BWANA akamkumbuka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kesho yake asubui, Elekana na jamaa yake waliamuka asubui mapema, na kisha kumwabudu Yawe, walirudi kwao Rama. Elekana akalala na muke wake Hana na Yawe akamukumbuka.