1 Samuel 1:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini safari hii Hana hakwenda, kwani alimwambia hivi mumewe, “Mara mtoto atakapoachishwa kunyonya, nitampeleka ili awekwe mbele ya Mwenyezi-Mungu, abaki huko daima.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hana hakuenda. Alimwambia mume wake, “Baada ya mtoto kuachishwa kunyonya, nitamchukua na kumpeleka mbele za Mwenyezi Mungu, naye ataishi huko daima.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bali Hana hakukwea; maana alimwambia mumewe, Sitakwea mimi hata mtoto wangu atakapoachishwa maziwa, hapo ndipo nitakapomleta, ili ahudhurie mbele za Bwana, akae huko daima.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini safari hii Hana hakwenda, kwani alimwambia hivi mumewe, “Mara mtoto atakapoachishwa kunyonya, nitampeleka ili awekwe mbele ya Mwenyezi-Mungu, abaki huko daima.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hana hakwenda. Alimwambia mume wake, “Baada ya mtoto kuachishwa kunyonya, nitamchukua na kumpeleka mbele za BWANA, naye ataishi huko wakati wote.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hana hakwenda. Alimwambia mume wake, “Baada ya mtoto kuachishwa kunyonya, nitamchukua na kumpeleka mbele za bwana, naye ataishi huko wakati wote.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bali Hana hakukwea; maana alimwambia mumewe, Sitakwea mimi hata mtoto wangu atakapoachishwa kunyonya, hapo ndipo nitakapomleta, ili awepo mbele za BWANA, akae huko daima.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini safari hii Hana hakwenda, kwani alimwambia hivi mumewe, “Mara mtoto atakapoachishwa kunyonya, nitampeleka ili awekwe mbele ya Mwenyezi-Mungu, abaki huko daima.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hana hakupanda nao, kwani alimwambia mumewe: Sharti huyu mwana kwanza aliache ziwa Kisha nitampeleka, amtokee Bwana usoni pake, akae hapo siku zote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bali Hana hakukwea; maana alimwambia mumewe, Sitakwea mimi hata mtoto wangu atakapoachishwa maziwa, hapo ndipo nitakapomleta, ili ahudhurie mbele za BWANA, akae huko daima.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini mara hii Hana hakuenda, maana alimwambia mume wake hivi: “Mara tu mutoto atakapoachishwa kunyonya, nitamupeleka kusudi awekwe mbele ya Yawe, abakie kule siku zote.”