1 Samuel 1:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Elkana, mumewe, akamjibu, “Fanya unaloona linafaa. Ngojea hadi utakapomwachisha mtoto kunyonya. Mwenyezi-Mungu aifanye nadhiri yako kuwa kweli.” Basi, Hana alibaki nyumbani, akaendelea kumlea mtoto wake hadi alipomwachisha kunyonya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Elkana mumewe akamwambia, “Fanya lile unaloona ni bora zaidi kwako. Ukae hapa hadi utakapomwachisha kunyonya, Mwenyezi Mungu na akujalie kutimiza nadhiri yako.” Hivyo huyo mwanamke akakaa nyumbani na kumnyonyesha mwanawe hadi alipomwachisha kunyonya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Elkana, mumewe, akamwambia, Haya, fanya uonavyo vema; ngoja hata utakapomwachisha maziwa; Bwana na alithibitishe neno lake tu. Basi yule mwanamke akangoja, akamnyonyesha mtoto wake, hata akamwachisha maziwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Elkana, mumewe, akamjibu, “Fanya unaloona linafaa. Ngojea hadi utakapomwachisha mtoto kunyonya. Mwenyezi-Mungu aifanye nadhiri yako kuwa kweli.” Basi, Hana alibaki nyumbani, akaendelea kumlea mtoto wake hadi alipomwachisha kunyonya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Elikana mumewe akamwambia, “Fanya lile unaloona ni bora zaidi kwako. Ukae hapa mpaka utakapomwachisha kunyonya, BWANA na akujalie kutimiza nadhiri yako.” Hivyo huyo mwanamke akakaa nyumbani na kunyonyesha mwanawe mpaka alipomwachisha kunyonya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Elikana mumewe akamwambia, “Fanya lile unaloona ni bora zaidi kwako. Ukae hapa mpaka utakapomwachisha kunyonya, bwana na akujalie kutimiza nadhiri yako.” Hivyo huyo mwanamke akakaa nyumbani na kumnyonyesha mwanawe mpaka alipomwachisha kunyonya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Elkana, mumewe, akamwambia, Haya, fanya uonavyo vema; ngoja hadi utakapomwachisha kunyonya; BWANA na alithibitishe neno lake tu. Basi yule mwanamke akangoja, akamnyonesha mtoto wake, hadi akamwachisha kunyonya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Elkana, mumewe, akamjibu, “Fanya unaloona linafaa. Ngojea hadi utakapomwachisha mtoto kunyonya. Mwenyezi-Mungu aifanye nadhiri yako kuwa kweli.” Basi, Hana alibaki nyumbani, akaendelea kumlea mtoto wake hadi alipomwachisha kunyonya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mumewe Elkana akamwambia: Yafanye yaliyo mema machoni pako! Kaa, mpaka umzoeze kuacha kunyonya! Naye Bwana na alitimize neno lako. Ndipo, mama ya mtoto alipokaa na kumnyonyesha mwanawe, mpaka akimzoeza kuacha kunyonya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Elkana, mumewe, akamwambia, Haya, fanya uonavyo vema; ngoja hata utakapomwachisha maziwa; BWANA na alithibitishe neno lake tu. Basi yule mwanamke akangoja, akamnyonyesha mtoto wake, hata akamwachisha maziwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mume wake Elekana, akamujibu: “Fanya unaloona linafaa. Ngojea mpaka utakapomwachisha mutoto kunyonya. Yawe afanye kiapo chako kuwa kweli.” Basi, Hana alibaki kwake, akaendelea kumulea mutoto wake mpaka alipomwachisha kunyonya.