1 Samuel 1:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila mwaka Elkana alisafiri kutoka Rama kwenda kuabudu na kumtambikia Mwenyezi-Mungu wa majeshi kule Shilo. Huko, watoto wawili wa kiume wa Eli, Hofni na Finehasi, walikuwa makuhani wa Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila mwaka mtu huyu alikwea kutoka mji wake ili kuabudu na kutoa dhabihu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni huko Shilo, ambapo Hofni na Finehasi, wana wawili wa Eli, walikuwa makuhani wa Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mtu huyo alikuwa akikwea kutoka mjini kwake mwaka kwa mwaka, ili kuabudu, na kumtolea Bwana wa majeshi dhabihu katika Shilo. Na wale wana wawili wa Eli, Hofni na Finehasi, makuhani wa Bwana, walikuwako huko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila mwaka Elkana alisafiri kutoka Rama kwenda kuabudu na kumtambikia Mwenyezi-Mungu wa majeshi kule Shilo. Huko, watoto wawili wa kiume wa Eli, Hofni na Finehasi, walikuwa makuhani wa Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila mwaka mtu huyu alikwea kutoka mji wake ili kuabudu na kutoa dhabihu kwa BWANA Mwenye Nguvu Zote huko Shilo, ambapo Hofni na Finehasi, wana wawili wa Eli, walikuwa makuhani wa BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila mwaka mtu huyu alikwea kutoka mji wake ili kuabudu na kutoa dhabihu kwa bwana Mwenye Nguvu Zote huko Shilo, ambapo Hofni na Finehasi, wana wawili wa Eli, walikuwa makuhani wa bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mtu huyo alikuwa akikwea kutoka mjini kwake mwaka kwa mwaka, ili kuabudu, na kumtolea BWANA wa majeshi dhabihu katika Shilo. Na wale wana wawili wa Eli, Hofni na Finehasi, makuhani wa BWANA, walikuwako huko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila mwaka Elkana alisafiri kutoka Rama kwenda kuabudu na kumtambikia Mwenyezi-Mungu wa majeshi kule Shilo. Huko, watoto wawili wa kiume wa Eli, Hofni na Finehasi, walikuwa makuhani wa Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yule mtu alitoka mwaka kwa mwaka mjini kwake akipanda kwenda Silo kumtambikia Bwana Mwenye vikosi na kumtolea ng'ombe ya tambiko. Huko wana wawili wa Eli, Hofuni na Pinehasi, walikuwa watambikaji wa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mtu huyo alikuwa akikwea kutoka mjini kwake mwaka kwa mwaka, ili kuabudu, na kumtolea BWANA wa majeshi dhabihu katika Shilo. Na wale wana wawili wa Eli, Hofni na Finehasi, makuhani wa BWANA, walikuwako huko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila mwaka Elekana alisafiri kutoka Rama kwenda kuabudu na kumutolea Yawe wa majeshi sadaka kule Shilo. Kule, wana wawili wa Eli, Hofuni na Finehasi, walikuwa makuhani wa Yawe.