1 Samuel 1:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mambo haya yaliendelea mwaka baada ya mwaka. Kila mara Hana alipokwenda kwenye nyumba ya Mwenyezi-Mungu, Penina alimkasirisha Hana hata ikawa Hana analia na kukataa kula chochote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hili liliendelea mwaka baada ya mwaka. Kila mara Hana alipoenda katika nyumba ya Mwenyezi Mungu, mke mwenzake alikuwa akimkasirisha hadi analia na kushindwa kula.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena mumewe akafanya hivyo mwaka kwa mwaka, hapo yule mwanamke alipokwea kwenda nyumbani kwa Bwana, ndivyo yule alivyomchokoza; basi, kwa hiyo, yeye akalia, asile chakula.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mambo haya yaliendelea mwaka baada ya mwaka. Kila mara Hana alipokwenda kwenye nyumba ya Mwenyezi-Mungu, Penina alimkasirisha Hana hata ikawa Hana analia na kukataa kula chochote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hili liliendelea mwaka baada ya mwaka. Kila mara Hana alipokwenda katika nyumba ya BWANA, mke mwenzake alikuwa akimkasirisha mpaka analia na kushindwa kula.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hili liliendelea mwaka baada ya mwaka. Kila mara Hana alipokwenda katika nyumba ya bwana, mke mwenzake alikuwa akimkasirisha mpaka analia na kushindwa kula.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena mumewe akafanya hivyo mwaka kwa mwaka, hapo yule mwanamke alipokwea kwenda nyumbani kwa BWANA, ndivyo yule alivyomchokoza; basi, kwa hiyo, yeye akalia, asile chakula.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mambo haya yaliendelea mwaka baada ya mwaka. Kila mara Hana alipokwenda kwenye nyumba ya Mwenyezi-Mungu, Penina alimkasirisha Hana hata ikawa Hana analia na kukataa kula chochote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, alivyofanya mwaka kwa mwaka: kila alipopanda kuingia Nyumbani mwa Bwana, yule alimsikitisha, hata akalia machozi na kukataa kula.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena mumewe akafanya hivyo mwaka kwa mwaka, hapo yule mwanamke alipokwea kwenda nyumbani kwa BWANA, ndivyo yule alivyomchokoza; basi, kwa hiyo, yeye akalia, asile chakula.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mambo hayo yaliendelea kila mwaka. Kila mara Hana alipokwenda kwenye nyumba ya Yawe, Penina alimukasirikisha Hana hata Hana akalia na kukataa kula chochote.