1 Samuel 10:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo Samueli akachukua chupa ndogo ya mafuta akammiminia Shauli kichwani, akambusu na kumwambia, “Mwenyezi-Mungu amekutia mafuta uwe mtawala juu ya watu wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Samweli akachukua chupa ndogo ya mafuta na kuyamimina juu ya kichwa cha Sauli, akambusu, akisema, “Je, Mwenyezi Mungu hakukupaka mafuta uwe kiongozi juu ya urithi wake?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Samweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina kichwani pake, akambusu, akasema, Je! Bwana hakukutia mafuta [uwe mkuu juu ya watu wake Israeli? Nawe utamiliki watu wa Bwana, na kuwaokoa na mikono ya adui zao; kisha hii itakuwa ishara kwako ya kuwa Bwana amekutia mafuta]
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo Samueli akachukua chupa ndogo ya mafuta akammiminia Shauli kichwani, akambusu na kumwambia, “Mwenyezi-Mungu amekutia mafuta uwe mtawala juu ya watu wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Samweli akachukua chupa ndogo ya mafuta na kuyamimina juu ya kichwa cha Sauli, akambusu, akisema, “Je, BWANA hakukutia mafuta uwe kiongozi juu ya watu wake Israeli?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Samweli akachukua chupa ndogo ya mafuta na kuyamimina juu ya kichwa cha Sauli, akambusu, akisema, “Je, bwana hakukutia mafuta uwe kiongozi juu ya watu wake Israeli?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Samweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina kichwani pake, akambusu, akasema, Je! BWANA hakukutia mafuta [uwe mkuu juu ya watu wake Israeli? Nawe utamiliki watu wa BWANA, na kuwaokoa kutoka katika mikono ya adui zao; kisha hii itakuwa ishara kwako ya kuwa BWANA amekutia mafuta] uwe mkuu juu ya urithi wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo Samueli akachukua chupa ndogo ya mafuta akammiminia Shauli kichwani, akambusu na kumwambia, “Mwenyezi-Mungu amekutia mafuta uwe mtawala juu ya watu wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Samweli alipokitwaa kichupa cha mafuta, akayamiminia kichwa chake, akamnonea midomo na kumwambia: Hivi ndivyo, Bwana anavyokupaka mafuta, uwe mkuu wao walio fungu lake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Samweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina kichwani pake, akambusu, akasema, Je! BWANA hakukutia mafuta [uwe mkuu juu ya watu wake Israeli? Nawe utamiliki watu wa BWANA, na kuwaokoa na mikono ya adui zao; kisha hii itakuwa ishara kwako ya kuwa BWANA amekutia mafuta] uwe mkuu juu ya urithi wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Samweli akatwaa chupa ndogo ya mafuta akamumiminia Saulo juu ya kichwa, akamubusu na kumwambia: “Yawe amekutia mafuta ukuwe mutawala juu ya watu wake.