1 Samuel 10:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipowasili aliwaambia, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Niliwatoa Waisraeli nchini Misri, nikawaokoa nyinyi kutoka kwa Wamisri na falme nyingine zilizowakandamiza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
naye akawaambia, “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli: ‘Niliwatoa Israeli kutoka Misri, nami niliwaokoa toka nguvu za Misri na falme zote zilizowadhulumu.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akawaambia wana wa Israeli, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Naliwatoa Israeli kutoka Misri, nami naliwaokoa ninyi na mikono ya Wamisri, na ya falme zote zilizowaonea;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipowasili aliwaambia, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Niliwatoa Waisraeli nchini Misri, nikawaokoa nyinyi kutoka kwa Wamisri na falme nyingine zilizowakandamiza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
naye akawaambia, “Hili ndilo asemalo BWANA, Mungu wa Israeli: ‘Niliwatoa Israeli kutoka Misri, nami niliwaokoa toka nguvu za Misri na falme zote zile zilizowaonea.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
naye akawaambia, “Hili ndilo asemalo bwana, Mungu wa Israeli: ‘Niliwatoa Israeli kutoka Misri, nami niliwaokoa toka nguvu za Misri na falme zote zilizowaonea.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akawaambia wana wa Israeli, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Niliwatoa Waisraeli kutoka Misri, nami niliwaokoa ninyi kutoka katika mikono ya Wamisri, na ya falme zote zilizowaonea;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipowasili aliwaambia, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Niliwatoa Waisraeli nchini Misri, nikawaokoa nyinyi kutoka kwa Wamisri na falme nyingine zilizowakandamiza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawaambia wana wa Isiraeli: Hivi ndivyo, anavyosema Bwana Mungu wa Isiraeli: Mimi niliwatoa Waisiraeli Misri, nikawaponya mikononi mwa Wamisri namo mikononi mwa wafalme wote waliowasumbua ninyi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akawaambia wana wa Israeli, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Naliwatoa Israeli kutoka Misri, nami naliwaokoa ninyi na mikono ya Wamisri, na ya falme zote zilizowaonea;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipofika aliwaambia: “Yawe, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Niliwatoa Waisraeli katika inchi ya Misri, nikawaokoa ninyi kutoka kwa Wamisri na falme zingine zilizowagandamiza.