1 Samuel 10:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akalileta mbele kabila la Benyamini, kulingana na koo zake, na ukoo wa Matri ukachaguliwa kwa kura. Mwisho akauleta mbele ukoo wa Matri, na Shauli mwana wa Kishi akachaguliwa kwa kura. Lakini walipomtafuta hakupatikana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha akalisogeza mbele kabila la Benyamini, kufuatana na koo zao, nao ukoo wa Matri ukachaguliwa. Mwishoni Sauli mwana wa Kishi akachaguliwa. Lakini walipomtafuta, hakuonekana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha akaileta kabila ya Benyamini karibu, kwa jamaa zao; jamaa ya Wamatri ikatwaliwa. Akaileta jamaa ya Wamatri karibu, mtu baada ya mtu; kisha Sauli, mwana wa Kishi, akatwaliwa; lakini walipomtafuta hakuonekana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akalileta mbele kabila la Benyamini, kulingana na koo zake, na ukoo wa Matri ukachaguliwa kwa kura. Mwisho akauleta mbele ukoo wa Matri, na Shauli mwana wa Kishi akachaguliwa kwa kura. Lakini walipomtafuta hakupatikana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha akalisogeza mbele kabila la Benyamini, ukoo kwa ukoo, nao ukoo wa Matri ukachaguliwa. Mwishoni Sauli mwana wa Kishi akachaguliwa. Lakini walipomtafuta, hakuonekana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha akalisogeza mbele kabila la Benyamini, ukoo kwa ukoo, nao ukoo wa Matri ukachaguliwa. Mwishoni Sauli mwana wa Kishi akachaguliwa. Lakini walipomtafuta, hakuonekana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha akalileta kabila la Benyamini karibu, kulingana na jamaa zao; jamaa ya Wamatri ikachukuliwa kwa kura. Akaileta jamaa ya Wamatri karibu, mtu baada ya mtu; kisha Sauli, mwana wa Kishi, akachaguliwa kwa kura; lakini walipomtafuta hakuonekana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akalileta mbele kabila la Benyamini, kulingana na koo zake, na ukoo wa Matri ukachaguliwa kwa kura. Mwisho akauleta mbele ukoo wa Matri, na Shauli mwana wa Kishi akachaguliwa kwa kura. Lakini walipomtafuta hakupatikana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha alipolifikisha shina la Benyamini milango kwa milango, ukashikwa mlango wa Matiri, kisha akashikwa Sauli, mwana wa Kisi. Lakini walipomtafuta hawakumwona.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha akaileta kabila ya Benyamini karibu, kwa jamaa zao; jamaa ya Wamatri ikatwaliwa. Akaileta jamaa ya Wamatri karibu, mtu baada ya mtu; kisha Sauli, mwana wa Kishi, akatwaliwa; lakini walipomtafuta hakuonekana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akalileta mbele kabila la Benjamina, kulingana na ukoo zake, na ukoo wa Matiri ukachaguliwa kwa kura. Mwisho akauleta mbele ukoo wa Matiri, na Saulo mwana wa Kisi akachaguliwa kwa kura. Lakini walipomutafuta hakupatikana.