1 Samuel 10:24 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Samueli akawaambia watu wote, “Huyu ndiye mtu aliyeteuliwa na Mwenyezi-Mungu katika watu wote; hakuna yeyote aliye kama yeye.” Watu wote wakapiga kelele: “Aishi mfalme.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Samweli akawaambia watu wote, “Je, mnamwona mtu ambaye Mwenyezi Mungu amemchagua? Hayupo aliye kama yeye miongoni mwa watu wote.” Ndipo watu wakasema kwa sauti kuu, “Mfalme aishi maisha marefu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Samweli akawaambia watu wote, Mnamwona mtu huyu aliyechaguliwa na Bwana, ya kuwa hakuna mtu mfano wake katika watu wote. Ndipo watu wote wakapiga kelele, wakasema, Mfalme na aishi!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Samueli akawaambia watu wote, “Huyu ndiye mtu aliyeteuliwa na Mwenyezi-Mungu katika watu wote; hakuna yeyote aliye kama yeye.” Watu wote wakapiga kelele: “Aishi mfalme.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Samweli akawaambia watu wote, “Je, mnamwona mtu ambaye BWANA amemchagua? Hayupo aliye kama yeye miongoni mwa watu wote.” Ndipo watu wakapiga kelele, wakasema, “Mfalme na aishi maisha marefu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Samweli akawaambia watu wote, “Je, mnamwona mtu ambaye bwana amemchagua? Hayupo aliye kama yeye miongoni mwa watu wote.” Ndipo watu wakapiga kelele, wakasema, “Mfalme na aishi maisha marefu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Samweli akawaambia watu wote, Mnamwona mtu huyu aliyechaguliwa na BWANA, kwamba hakuna mtu mfano wake katika watu wote. Ndipo watu wote wakapiga kelele, wakasema, Mfalme na aishi!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Samueli akawaambia watu wote, “Huyu ndiye mtu aliyeteuliwa na Mwenyezi-Mungu katika watu wote; hakuna yeyote aliye kama yeye.” Watu wote wakapiga kelele: “Aishi mfalme.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Samweli akawaambia watu wote: Mmemwona, Bwana aliyemchagua? Kwani kwao watu wote hakuna afananaye naye. Ndipo, wote walipopiga yowe za kumshangilia kwamba: Pongezi, mfalme!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Samweli akawaambia watu wote, Mnamwona mtu huyu aliyechaguliwa na BWANA, ya kuwa hakuna mtu mfano wake katika watu wote. Ndipo watu wote wakapiga kelele, wakasema, Mfalme na aishi!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Samweli akawaambia watu wote: “Huyu ndiye mutu aliyechaguliwa na Yawe kati ya watu wote; hakuna yeyote anayekuwa kama yeye.” Watu wote wakapiga kelele: “Mufalme aishi milele.”