1 Samuel 10:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, Samueli aliwaeleza watu juu ya wajibu na haki za mfalme, akaziandika katika kitabu ambacho alikiweka mbele ya Mwenyezi-Mungu. Kisha, Samueli aliwaaga watu wote, kila mtu aende nyumbani kwake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Samweli akawaeleza watu madaraka ya ufalme. Akayaandika kwenye kitabu na kukiweka mbele za Mwenyezi Mungu. Kisha Samweli akawaruhusu watu kila mmoja aende nyumbani mwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha Samweli aliwaambia watu madaraka ya ufalme, akayaandika katika kitabu, akakiweka mbele za Bwana. Samweli akawaruhusu watu wote, waende kila mtu nyumbani kwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, Samueli aliwaeleza watu juu ya wajibu na haki za mfalme, akaziandika katika kitabu ambacho alikiweka mbele ya Mwenyezi-Mungu. Kisha, Samueli aliwaaga watu wote, kila mtu aende nyumbani kwake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Samweli akawaeleza watu madaraka ya ufalme. Akayaandika kwenye kitabu na kuweka mbele za BWANA. Kisha Samweli akawaruhusu watu, kila mmoja aende nyumbani kwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Samweli akawaeleza watu madaraka ya ufalme. Akayaandika kwenye kitabu na kuweka mbele za bwana. Kisha Samweli akawaruhusu watu, kila mmoja aende nyumbani kwake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha Samweli aliwaambia watu kazi ya ufalme, akayaandika katika kitabu, akakiweka mbele za BWANA. Samweli akawaruhusu watu wote, waende kila mtu nyumbani kwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, Samueli aliwaeleza watu juu ya wajibu na haki za mfalme, akaziandika katika kitabu ambacho alikiweka mbele ya Mwenyezi-Mungu. Kisha, Samueli aliwaaga watu wote, kila mtu aende nyumbani kwake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Samweli akawaambia watu haki yake mfalme, akaiandika katika kitabu, akakiweka hapo pake Bwana; kisha Samweli akawaaga watu wote, waende zao kila mtu nyumbani kwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha Samweli aliwaambia watu madaraka ya ufalme, akayaandika katika kitabu, akakiweka mbele za BWANA. Samweli akawaruhusu watu wote, waende kila mtu nyumbani kwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, Samweli aliwaelezea watu juu ya mapaswa na haki za mufalme, akaziandika katika kitabu ambacho alikiweka mbele ya Yawe. Kisha, Samweli aliwaaga watu wote, kila mutu aende kwake.