1 Samuel 11:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha mfalme Nahashi wa Waamoni, alikwenda na kuuzingira mji wa Yabesh-gileadi. Wakazi wa mji wa Yabesh-gileadi wakamwambia Nahashi, “Fanya mapatano nasi, nasi tutakutumikia.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nahashi Mwamoni akakwea kuuzingira mji wa Yabesh-Gileadi kwa jeshi. Wanaume wote wa Yabeshi wakamwambia, “Fanya mkataba nasi, na tutakutumikia.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa, kama baada ya mwezi mmoja, Nahashi,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha mfalme Nahashi, wa Waamoni. alikwenda na kuuzingira mji wa Yabesh-gileadi Wakazi wa mji wa Yabesh-gileadi wakamwambia Nahashi, “Fanya mapatano nasi, nasi tutakutumikia.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nahashi, Mwamori, akakwea kuuzunguka kwa jeshi mji wa Yabeshi-Gileadi. Watu wote wa Yabeshi wakamwambia, “Fanya mkataba na sisi, na tutakuwa chini yako.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nahashi yule Mwamoni, akakwea kuuzunguka kwa jeshi mji wa Yabeshi-Gileadi. Watu wote wa Yabeshi wakamwambia, “Fanya mkataba na sisi, na tutakuwa chini yako.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa, kama baada ya mwezi mmoja, Nahashi, Mwamoni, akakwea na kupiga kambi juu ya Yabesh-gileadi; na watu wote wa Yabeshi wakamwambia Nahashi, Fanya mapatano nasi, na sisi tutakutumikia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha mfalme Nahashi wa Waamoni, alikwenda na kuuzingira mji wa Yabesh-gileadi. Wakazi wa mji wa Yabesh-gileadi wakamwambia Nahashi, “Fanya mapatano nasi, nasi tutakutumikia.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nahasi wa Waamoni akapanda, akapiga makambi huko Yabesi katika nchi ya Gileadi. Ndipo, watu wote wa Yabesi walipomwambia Nahasi: Fanya agano nasi, tukutumikie!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa, kama baada ya mwezi mmoja, Nahashi, Mwamoni, akakwea na kupanga marago juu ya Yabesh-gileadi; na watu wote wa Yabeshi wakamwambia Nahashi, Fanya mapatano nasi, na sisi tutakutumikia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme Nahasi wa Waamoni, alikwenda na kuushambulia muji wa Yabesi-Gileadi. Wakaaji wa muji wa Yabesi-Gileadi wakamwambia Nahasi: “Fanya mapatano nasi, nasi tutakutumikia.”