1 Samuel 11:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini akawaambia, “Nitafanya mapatano nanyi kwa sharti moja kwamba nitamngoa kila mmoja wenu jicho lake la kulia; hivyo nitawaaibisha Waisraeli wote.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Nahashi yule Mwamoni akajibu, “Nitafanya mkataba na ninyi tu kwa sharti kwamba nitang’oa jicho la kulia la kila mmoja wenu, na hivyo kuleta aibu juu ya Israeli yote.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Huyo Nahashi, Mwamoni, akawaambia, Kwa sharti hii mimi nitapatana nanyi, kila mtu ang'olewe jicho la kuume; na kwa jambo hilo nitawashutumu Waisraeli wote pia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini akawaambia, “Nitafanya mapatano nanyi kwa sharti moja kwamba nitamng'oa kila mmoja wenu jicho lake la kulia; hivyo nitawaaibisha Waisraeli wote.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Nahashi, Mwamori, akajibu, “Nitafanya mkataba na ninyi tu kwa sharti kwamba nitang'oa jicho la kulia la kila mmoja wenu, na hivyo kuleta aibu juu ya Israeli yote.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Nahashi yule Mwamoni akajibu, “Nitafanya mkataba na ninyi tu kwa sharti kwamba nitang’oa jicho la kulia la kila mmoja wenu, na hivyo kuleta aibu juu ya Israeli yote.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Huyo Nahashi, Mwamoni, akawaambia, Kwa sharti hili mimi nitapatana nanyi, kila mtu ang'olewe jicho la kulia; na kwa jambo hilo nitawashutumu Waisraeli wote pia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini akawaambia, “Nitafanya mapatano nanyi kwa sharti moja kwamba nitamngoa kila mmoja wenu jicho lake la kulia; hivyo nitawaaibisha Waisraeli wote.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwamoni Nahasi akawaambia: Basi, nitapatana nanyi hivyo: nitawachoma ninyi kila mtu jicho lake la kuume, niwatweze Waisiraeli wote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Huyo Nahashi, Mwamoni, akawaambia, Kwa sharti hii mimi nitapatana nanyi, kila mtu ang’olewe jicho la kuume; na kwa jambo hilo nitawashutumu Waisraeli wote pia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini akawaambia: “Nitafanya mapatano nanyi kwa shurti hii moja: nitamwongoa kila mumoja wenu jicho lake la kuume. Hivyo nitawapatisha Waisraeli wote haya.”